Kujiegemeza kwa PM wa UK Rishi Sunat ni hadithi ile ile ya matusi tuliyomtukana Obama

Kujiegemeza kwa PM wa UK Rishi Sunat ni hadithi ile ile ya matusi tuliyomtukana Obama

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Waafrika tuna ufundi mwingi wa kujihusianisha na watu maarufu wenye madaraka makubwa huko Ulaya na US. Mtu hata anayeonekana kama ni mchovu tu akianza kuongea atataka awatishe wanaomsikiliza kwa kuchomekea mbwembwe za hapa na pale ili mradi tu aonekane ni wa maana kwa wanaomsikiliza.

Ni suala linaloanzia mbali kwenye asili yetu, kupenda kumjua mtoto wa fulani ili uwatambie wenzako mtaani. Kupenda kuwa karibu na mtu fulani mwenye cheo ili akupe urahisi wa kutatua matatizo yako mbalimbali.

Ni hapa zile simulizi zetu maarufu za 'nilisoma na mtoto wa Warioba darasa moja pale Shaban Robert" au mwingine atasema 'chuo kikuu nilikuwa darasa moja na Kikwete pale Mlimani' majigambo yote haya ni hulka yetu ya kiafrika ya muda mrefu.

Mama yake waziri mkuu mpya wa UK alizaliwa Tanzania na alikulia miaka ya mwanzo ya uhai wake huko Shinyanga, vinatembea vibonzo vya kumuweka karibu na Tanzania mtoto wake aliyepata madaraka makubwa.

Ni kama vile vibonzo vya Obama kwamba Baba yake ni Mkenya asili hivyo afrika itapata kitu fulani kutoka kwake!. Haya yalikuwa ni mawazo ya wakati ule alipoingia White House. Baada ya miezi miwili ya mwanzo ndio wakenya waliojisifu ujaluo wa Obama wakatambua kuwa yeye kwanza ni Mmarekani kabla hajawa Mkenya, anatekeleza sera na mitazamo ya kimarekani kwanza.

Miaka ikapita na ule mteremko walioutegemea kutoka kwa Obama ukawa hauonekani kuleta neema kwa afrika na Kenya kwa ujumla!. Alipomaliza miaka ya urais wake akafanya ziara ya binafsi kutembelea familia yake ya Kenya na wakati huo Kaka yake akamsema vibaya mdogo wake kwamba haijali familia ya asili yake.

Huyu PM mpya wa Uingereza ni mhindi kama walivyo watu wengi wenye asili ya India, hategemewi hata chembe kuipa kipaumbele Tanzania yenye mkoa wa Shinyanga eti kwa kigezo kuwa Mama yake amezaliwa eneo lile. Hawa ni watu wa kimataifa zaidi, wamejua namna ya kuvizia fursa tangu miaka hiyo ya mwanzo wa karne iliyopita.

Kila la kheri PM Sunat katika kazi yako mpya iliyojaa changamoto nyingi na ngumu kuzitatua.
 
Mtu kusema kuwa alisoma na fulani ambaye sasa ni rais, waziri zu mkubwa, fulani hiyo ni fact na ikisemwa sio kujitafutia umaarufu. Historia,ya mtu maarufu kuwa imefungamana na mtu au jamii fulani ikiekezwa sio kosa ni ukweli na itabaki kuwa ukweli.
 
Waziri Mkuu wa kwanza wa UK mwenye asili ya Bara hindi.

Labda huyu ataleta dialogue na Warusi.
Na ukweli ndiyo huu! Huyo ni Waziri Mkuu wa Uingereza, mwenye asili ya India.

Haya mambo ya mama yake sijui alizaliwa Tanzania, sijui baba yake alikulia Kenya!! haiondoi ukweli wa huyo jamaa kuwa na asili ya India.
 
Mtu kusema kuwa alisoma na fulani ambaye sasa ni rais, waziri zu mkubwa, fulani hiyo ni fact na ikisemwa sio kujitafutia umaarufu. Historia,ya mtu maarufu kuwa imefungamana na mtu au jamii fulani ikiekezwa sio kosa ni ukweli na itabaki kuwa ukweli.
Inategemea na jinsi hiyo taarifa inawasilishwa. Ukitaarifu tu kuwa ulisoma na mtu maarufu hiyo ni sawa.
Tatizo linakuja pale unapotumia taarifa hiyo kama vile ni jambo la muhimu sana katika kukuwakilisha wewe kama mtu wa muhimu. Na hii ndio wengi wanayo, kuwa "unaniangalia kwa uoga mimi nimesoma na fulani".
 
Back
Top Bottom