wa kibondemaji
Member
- Aug 1, 2024
- 30
- 53
Habari wana-JamiiForums,
Nina umri wa miaka 27 ni muajiriwa wa serikali tangu mwaka 2023 nikiwa kama afisa tabibu (clinical officer). Nimeleta uzi huu kwenu nikiomba ushauri kuna mambo kama mawili natamani kuyafanya la kwanza ni kujiendeleza kielimu na la pili ni kufanya biashara vyote nikiwana lengo la kujikwamua kiuchumi.
Sasa kinachoniweka dilema ni kwamba nianze na kipi kati ya elimu au biashara, na je kama ni elimu nitasoma kozi ipi ambayo itanipa fursa either kupanda ngazi zaidi au kupitia elimu hiyo nitakayoipata niweze kufanya mambo yangu binafsi? Na je, endapo nikipata kozi haihusiani na fani yangu ya sasa. Je, itawezekana kubadili fani?
Pili kuhusu biashara kutokana mazingira niliyopo ya kazi sio rahisi kufanya biashara kubwa au biashara ya kupiga hatua ambayo mimi natamani kufanya hivyo itanibidi either nihame au nifungue sehemu nyingine na je vipi kuhusu management ya hiyo biashara?
Maana kuna biashara niliwaza kufanya mfano kufungua shule ya watoto, kufungua zahanati au maabara au pharmacy, biashara ya vinywaji kama bia na pombe kali na biashara ya vipodozi. Lakini pia fursa nyingine iliyopo huku ni kama uvuvi japo kwa asilimia ndogo na pia kilimo lakini changamoto ni kubwa kama wanyamapori kuvamia mashamba, mafuriko nk