SoC01 Kujikuta utumwani kwenye ndoto ya uhuru

Stories of Change - 2021 Competition

msakhara

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2019
Posts
277
Reaction score
381
Viumbe vyote ulimwenguni vina asili inayofanana sana. Viumbe vyote vinahitaji kukua na vinahitaji uhuru katika ukuaji huo.

Kwa binadamu pia kama sehemu ya viumbe wengine ukuaji ni jambo la msingi. Binadamu anahitaji kukua kijamii, kiuchumi na kibaiolojia ili kwendana na mabadiliko ya mazingira yanayomzunguka.

Kukosa ukuaji, au kuwa na ukuaji hafifu katika nyanja zote tajwa hapo juu huchukuliwa kama maumivu kwa hisia za kibinaadamu.

Ili kuepuka maumivu haya, binadamu hujiuliza (kwa kujua au kuto kujua) ni namna gani atakwepa udumavu na kukosa uhuru?

Ni namna gani atakua katika hatua ambayo jamii inataka awe?
Ni njia zipi atatumia kuipata kesho iliyo bora zaidi ya leo?

Katika harakati za kutafuta majibu ya maswali haya, kuna baadhi ya watu na taasisi zinatumia fursa, kwa kutatua changamoto za watu katika hatua zao za ukuaji na uhuru.

Miongoni mwa taasisi nyingine, ni taasisi za kifedha na ukopeshaji.
Taasisi hizi hukopesha fedha kwa watu ili kuwasaidia kufikia malengo na hatua mbalimbali za maisha yao kwa kutoa huduma mbalimbali. Huduma moja wapo ni kutoa mikopo kwa wateja wake ili kuwasaidia kutimiza malengo mbalimbali.

Kuna wanaokopa ili kujenga nyumba, kuanzisha biashara, kupeleka watoto shule nzuri, kumiliki gari kali n.k.

Watu wengi hukopa ili kukua (kiuchumi) na kuwa huru machoni pa jamii inayowazunguka.

Katika kutafuta uhuru huo, watu wengi wamejikuta wakijitia katika vifungo vya kiuchumi kwa sababu ya mikopo hii kwa sababu mbalimbali. Watu wamejikuta wakiuziwa nyumba zao, wakiuziwa mashamba ,kufirisiwa, na baadhi ya vitu vya familia kuuzwa ili kulipa mikopo.

Baadhi ya sababu zinazoweza pelekea kutokea kwa haya ni;

I. Kukopa bila kuwa na lengo maalum juu ya matumizi ya mkopo husika.
- Kunawatu huchukua mkopo bila ya kuwa na dhumuni thabiti la nini atafanyia hela hiyo!. Yaani mtu anakopa, baada ya hapo ndio anaanza kutafuta afanye biashara gani? Ajenge wapi? Aanzie wapi?
Wengi hujikuta wanajiingiza kwenye 'project' isiyolipa ama isiyoendana na uhalisia wa uchumi wake na kupelekea kutofauru na kuathiriwa na masharti ya mkopo.

II. Kukopa kwa malengo yasiyo rafiki kwa marejesho
- Baadhi ya watu hukopa kwa malengo yasiyo rafiki kwa urejeshaji wa fedha ya mkopo. Mf. Kununua gari asiyoweza kuimudu, kupeleka watoto shule zenye gharama kubwa ukilinganisha na kipato hivyo kupelekea kuumaliza fedha bila ya kuwa na njia yoyote ya marejesho na haimaye kuangukia kwenye kifungo cha kiuchumi

III. kukopa bila ya kujua kiundani masharti na riba za mkopo husika
- Kundi hili hukopa kwa kufuata mkumbo mf. "Rafiki yangu kakopa ngoja nami nikope " bila ya kuwa na wazo au lengo la muhimu juu ya matumizi ya fedha hiyo na baadaye kuishia kuiharibu.

IV. Tamaa na kukosa nidhamu ya fedha
- Kuna watu hukopa kwa lengo zuri, na mipango kedekede juu ya fedha ya mkopo. Baada ya muda huingiwa na tamaa na kutumia fedha nje ya kusudi lake na kusababisha kutotimiza lengo husika. Watu hao hushtuka wakiwa kwenye utumwa wa deni lao.

V. Ajali/ bahati mbaya
Kunawatu huwa na wazo zuri na lengo zuri ila hupatwa na majanga yasiyotegemewa hivyo kupoteza uwezo wa kulipa. Na kuishia kuwa watumwa wa deni

Ni muhimu sana kuzingatia mambo haya kabla hujachukua mkopo

I. Ijue vizuri taasisi inayokopesha , masharti na utamaduni wake

II. Elewa utaratibu wa malipo, riba na faida za kukopa taasisi husika

III. kuwa na lengo na mpango mathubuti wa matumizi ya mkopo unaopanga kuuchukua

IV. Jua namnagani utaurejesha mkopo wako kwa wakati muafaka

V. Tumia mkopo kwenye vitu vinavyoweza kukuingizia kipato au kupunguza sana matumizi ya awali ya fedha kwa sasa na baadaye.

VI. Usikope ili kuanzisha biashara, kopa ili kuendeleza biashara

VII. Omba kuepushwa na majanga na bahati mbaya zilizo nje ya uwezo wetu binaadam

VII. Zingatia (kwa wafanyakazi) makato ya mkopo yasiathiri sana pato lako hadi ukakosa hela ya kujikimu kibinaadamu na kuifanya familia nzima iteseke kwa kifungo chako cha kiuchumi.

Jitahidi mkopo iwe ni ushindi kwa pande zote, yaani faida kwa wakopeshaji na uhuru na ukuaji kiuchumi kwa wewe mkopaji.
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…