SoC04 Kujikwamua kiuchumi ndani ya miaka 10 hadi 20

SoC04 Kujikwamua kiuchumi ndani ya miaka 10 hadi 20

Tanzania Tuitakayo competition threads

Fauya

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2017
Posts
262
Reaction score
479
Habari yako ndugu msomaji wa chapisho hili,

Ninapenda kushirikisha maono yangu juu ya nini cha kufanya kwako kijana au mzee mtu mwenye umri wowote inakuhusu hii. Kuna baadhi mtaona kuwa miaka 10 ni mingi lakini kiuhalisia sio mingi.

Kwa mtu ambae miaka kumi iliyopita alimaliza kidato cha nne anaweza akawa shuhuda kwamba miaka kumi sio mingi kwani huu ndo mwaka wa 10 tangu amalize elimu ya kidato cha nne.

Twende kwenye mada nayotaka kuishirikisha hapa ni kwamba kama ukiweka mipango yako ya kujiletea maendeleo ndani ya miaka 10 utakua umefika mbali, kwa mfano wewe ni muajiriwa wa serikali unayechukua mshahara (take home) laki saba unaweza ukaanza ujenzi wa nyumba yako ya kupangisha au ya biashara au nyumba ya kuishi kwa kutumia milioni tatu kila mwaka katika lengo lako hilo, ambapo ndani ya miaka 10 utakua umetumia milioni thelathini. Na sehemu utakayoamua kujenga mda huu itakua ni kijijini hapajaendelea sana lakini baada ya miaka 10 patakua na utofauti patakua pameendelea kidogo.

Mradi mwingine unaoweza kujipanga uufanye kuanzia sasa ili ndani ya miaka 10 uwe umefanikiwa kimaisha ni ufugaji, kwa mfano ufugaji wa nguruwe (kwa wale dini inayoruhusu). Ukiwa na nguruwe wako wanne wa kuanzia mwaka huu unaweza ukakaa nao mwaka mzima ukawa unawahudumia vizuri baada ya mwaka ukawauza na ukapata faida ambayo hiyo faida unaweza ukaongezea na pesa nyingine unazozipata katika shughuli zako za kila siku mpaka pesa ikafikia mara mbili ya ile uliyoanzia na ukanunua watoto wengine wa nguruwe idadi ya watoto nane baada ya mwaka wakishafaa kuliwa ukawauza tena.

Lakini pia unaweza ukafanya biashara ya kuwazalisha nguruwe, mfano ukiwa na nguruwe wako wawili majike makubwa ukayapandishia dume yakabeba ujauzito kila mmoja kwa kiwango cha chini anaweza akazaa watoto sita hivyo jumla unakua na watoto 12 na kwa mwaka mmoja nguruwe hao wana uwezo wa kuzaa mara mbili hivyo kwa mwaka utakua na watoto 24 ambapo unaweza ukawauza miezi mitatu baada ya kizaliwa au kama una mpunga wa kutosha unaweza ukawatunza mpaka wakawa nguruwe wakubwa na ndo ikawa mwanzo wa kukuza biashara yako.

Mimi sina utaalamu sana wa kufanya hesabu za faida na hasara lakini wewe kama mwekezaji au mjasiriamali uliyejikita katika biashara mojawapo unapaswa ujue namna ya kutunza kumbukumbu zako kwa ajili ya kupiga hesabu za faida na hasara.
Kuna watu hawawezi kufanya biashara wanaona ni ngumu sana kufanya biashara, watu wa aina hii kuna mawili moja waishi maisha ya kawaida ya kutegemea mshahara na pale nguvu ya ufanyaji kazi itapoisha watakuwa maskini lakini, mbili mtu wa aina hii awekeze asilimia kadhaa ya mshahara wake ili atakapokuja kustaafu au nguvu kazi yake itapoisha aweze kupata fedha ya kuendeshea maisha yake.

Namna hii ya pili unaweza kuifanya kwa kuweka pesa zako katika mifuko ya uwekezaji na saccos lakini pia unaweza kutunza kiasi kadhaa cha mshahara wako alafu ukaja kuitumia hiyo akiba kununua hisa katika kampuni mbili au tatu kubwa na ukawa unapokea faida kila baada ya kipindi fulani kulingana na kampuni yenyewe.

Ndugu zangu ambao bado hamjafahamu namna ya kufanikiwa kimaisha nawaombeni msiwazie leo tuu bali wazeni miaka kadhaa mbele utakua katika hali gani. Kwa mfano kama mwaka huu ni wa kwako wa 27, waja je nikifikisha miaka 37 mtu akanipa milioni 10 je si atakua amenisaidia sana. Sasa hiyo milioni 10 unaweza ukajitengenezea kuanzia sasa kwa kutunza kila mwezi laki moja tuu.

Nawasilisha
 
Upvote 4
Mawazo mazuri kijana.
Pia unaweza kuzingati haya yafuatayo ktk kuweka malengo yako:-
1. Planning (Kuweka Malengo)
2. Goal setting (Kuweka mikakati ya kufikia malengo, simple translation)
3. Recording of the above two stages ( Kuandika hatua 1 & 2)
4. Evaluations quarterly ( Kuafanya tathmini kila baada ya miezi mitatu)
 
Back
Top Bottom