SoC01 Kujilinda dhidi ya mpenzi ya uongo kwa watoto wa kike

SoC01 Kujilinda dhidi ya mpenzi ya uongo kwa watoto wa kike

Stories of Change - 2021 Competition

Nester Reuben

New Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
3
Reaction score
6
Kujilinda dhidi ya mpenzi ya uongo kwa watoto wa kike

=====


KUJILINDA DHIDI YA MAPENZI YA UONGO KWA WATOTO WA KIKE
Na: Nester Reuben

Kwa muda mrefu sana kumekuwa na changamoto ya sisi watoto wakike kushindwa kuzielezea hisia tulizonazo kwa watu tunaowapenda kutokana na desturi iliyopo katika jamii eetu za Kiafrika. Tumekuwa tunashindwa kumtamkia mtu kuwa tunampenda kwa lengo la kuogopa kuonekana kuwa tunatabia mbaya (Malaya), hivyo tumekuwa tukiangukia kwenye mikono ya watu wasio sahihi kwetu.

Kutokana na hali hiyo tumejikuta tukiingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na watu ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa sio sahihi kwetu pia tunaanza kupata mashaka juu ya upendo wao kwetu na kushindwa kutambua kuwa wanatupenda kweli ua wanatuhitaji kwa malengo ya dhati lakini tunajikuta tukiingia kwenye wakati mgumu sana kwa kuanza kuhofia kwamba tunaweza kuanzisha mahusiano nao kwa lengo la kutakakutuchezea hivyo muda mwingi tunakuwa tunahisi kudanganywa tu.

Pia kadri siku zinavyozidi kwenda ndio mambo yanavyozidi kubadilika kabisa hasa kwa sisi ambao bado hatujabahatika kupata ndoa, kwani wanaume wa kizazi hiki wamakuwa na dhana potofu na hawanahofu ya Mungu sio wote lakini wengi wamejikita katika kitanzi cha kuwa tegemezi kwa wanawake zao.

Hivyo wamekuwa wanapenda sana wanawake ambao tayari wameimalika kiuchumi huwa wanawaingia wanawake hao bila kujali umri wao wala dni zao zaidi wao wanachokiangalia zaidi ni uchumi wao.

Hapo ndipo utaona mwanaume anakuwa anaigiza kukupenda sana kwakuwa mapenzi siku zote ni upofu nawe utaweza mpenda pia kwa sababu kwa siku za mwanzo anaweza kuja kwako kwa maneno mazuri na mipango mizuri na wewe na zawadi za hapa na pale mituko ya kila sehemu wakati huo yeye anakuwa anajua gharama zake zitarudije kwake pasipo wewe kujua wakati huo wewe unakuwa unahisi ni starehe tu.

Hapo sasa ndio utaona kuwa unapendwa sana na kufurahia mapenzi yake kwani lengo lake kubwa linakuwa kukufulahisha wewe kwa hiyo muda mwingi utakuwa naye, mara nyingi wanaume wa aina hii wengi wao wanakuwa hawana kazi maalum (Wazugaji) hivyo muda mwingi anakuwa karibu yako.
Jinsi ya kumjua Mkaka mwenye tabia hizo

Hapo unatakiwa kuwa makini sana yaani hakikisha kila ukiwa karibu naye jitahidi sana kumletaa mada za maendeleo na kila mtu apate nafasi ya kuongea juu ya malengo yake binafsi, japo kuwa watu hawa wanakuwa waongo waongo sana anaweza kukupa mipango yake na ukaona sawa, huyu ndio mtu niliyekuwa namuhitaji kwa muda mrefu sana na ukamshukuru Mungu kwa ajili yake.

Naongea hivi kwani nishawahi kukutana na mtu wa aina hiyo na nilipokutana naye kwa wakati huo tayari nilikuwa najua kuwa kuna watu wa haina hiyo kwani nishakuwa na rafiki yangu wakike ambaye alikuwa na mpenzi wake ambaye muda mwingi alikuwa anategemea pesa za rafiki yangu huyo kwa kiwango kikubwa sana na kumshawishi kuwa yeye ndiye mwanaume wa maisha yake kwahiyo asiwe na shaka nayeye kwani maendeleo yao wanayatafuta pamoja na siku akipata kazi basi atarudisha gharama zote alizozitumia kutoka kwa rafiki yangu.

Kwahiyo kwangu sikutumia nguvu kubwa sana kumtambua mtu mwenye tabia hiyo na niligundua kwa haraka zaidi.

Alikuwa ni mtu mwenye kuonesha kunijali sana na kuonesha anavivu na mimi kiasi kwamba nikawa nahisi yeye ndiye sahihi kwangu lakini kila baada ya siku hadi siku nikawa naona utofauti fulani hivi kwenye maongezi yake yaani alikuwa nimtu mwenye mipango zaidi lakini mipango yake hiyo ikawa haizai matunda.

Nikaanza kubadilika taratibu akiniita kwenye sehemu za starehe nikawa siendi maana ukienda basi bili ya pale utailipa wewe nayeye mara adanganye kuwa kadi yake imemezwa mara akupe kadi yake ambayo haina pesa anakupa tu kwa lengo la kukuchukua pesa. Lakini kwangu akawa akinipa kadi yake basi muda huo huo naenda nayo ATM iliyokaribu na hapo tulipo kisha naangalia salio mara ya kwanza nikakuta hakuna pesa kabisa.

Niliporudi nikamuuliza mbona akaunti yako haina pesa alinijibu kuwa ooh! Aisee bahati mbaya kadi yenye pesa nimesahau nyumbani basi hapo nikawa na mashaka naye
Kuna siku alitoka na rafiki zake wakanywa sana kisha akanipigia simu majira ya saa 4 hivi usiku nimfuate sehemu alipo ili turudi nyumbani kwa madai kuwa amelewa sana na hawezi kurudi kwake mwenyewe, kwa haraka haraka nikawaza nakuona sio sawa yaani mtu alewe kiasi kwamba ashindwe kurudi nyumbani kwake….

Nikajisemea mwenyewe sawa alivyokuwa hayuko na mimi akilewa alikuwa anarudishwa na nani? Basi hapo hapo nikazima simu, pia nikahisi atakuwa hana pesa ya usafiri wa kumrudisha nyumbani kwake kwahiyo anahitaji usafiri nitakaoenda nao pale ndio tutumie wote sababu bili lazima iwe kwangu kwakuwa mimi ndiye nitakaye kuwa nimepeleka pale, nilichokifanya kwa haraka haraka nikazima simu kisha nikalala.

Kuna muda anawezakukupia simu na kukueleza mipango ya pesa mkaongea kwa muda mrefu kisha mwisho wa maongezi anakukopa pesa na niyafanya kumkopesha kama mara mbili hivi lakini hakuwahi kunirudishia, japo alirudisha kwa njia nyingine ambayo na mimi nilimkopa pia nakumuonesha kuwa ninashida sana basi nikamshauri anikopee hata kwa rafiki zake kisha nitarudisha baada ya siku tatu namipia sikumrudishia japo kuwa haikuwa kama ninayomdai mimi.

Mimi nilikuwa namdai nyingi zaidi
Kuna siku aniita sehemu tuongee kwani alisema anashida sana na mtu wa kumsaidia ni mimi japo anajua kuwa namdai ila natakiwa kumsaidia kwani anashida sana. Baada ya kufika pale akaanza ninidanganya kuwa baba ake anaumwa sana anahitaji kufanyiwa upasuaji hivyo anahitaji kama pesa kwa ajili ya matibabu hayo.

Aisee kwa kweli sikuwa na cha kumwambia zaidi ya sina pesa pia alijitahidi sana kunishawishi ili nikakope pesa kwa dada yangu ili tumsaidie na hiyo ndio ilikuwa njia yangu ya mwisho ya kumchunguza na kujua lengo lake kwangu. Na sikusita kuchukua hatua zangu biafsi

Nb. Akuwahi kuacha kunijali wala kunifuatilia hata pale nilipogundua kuwa alikuwa ananitumia pia nilipogundua lengo lake sikuacha kukaa naye na kuongea naye juu ya tabia yake, nashukuru kwa kuwa aliniahidi kubadilika na kuacha kabisa tabia ya kutegemea wanawake

Hivyo:-
Tujitahidi sana kuondoka kwenye upofu wa mapenzi ya aina hii maana hawa watu siku hizi wamekuja na mbinu nyingine ambayo hawana hofu kabisa na mbinu hii mpya, akiona tu unaweza kumuudumia yeye basi ashindwi kukupa na ujauzito ambapo anakuwa anaamini sana kuwa ukiwa mama mtoto wake inakuwa ni ngumu sana kuamini kuwa anakutumia kwa kuwa wanawake wengi sana tunadhana potofu ya kuhisi kuwa mwanaume akikupa ujauzito basi anakuwa anakupenda na zamani ilikuwa hivyo wanaume wengi sana walikuwa na hofu ya kuogopa kumpa ujauzito mwanamke ambaye sio mkeo wake lakini saivi kuzaa imekuwa kitu cha kawida sana.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom