Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,339
- 3,667
Habarini wana Jamii Forums
Leo ningependa kuzungumza Pamoja na wanajamii wenzangu juu ya jambo moja ambalo limekuwepo katika jamii yetu siku nyingi na namna ambavyo linaweza kuwa pingu katika ustawi wetu na maendeleo yetu katika jami.KULINGANISHA
Nimekufananisha Kulinganisha na pingu kwa sababu, tunapoendelea kulinganisha na uwezo wetu na uwezo wa mtu au watu wengine tunakuwa ni kama tumefungiwa kwenye kufikiria kwetu,mamuzi yetu au hata hatua zetu kwa kuwa tukijilinganisha mara kwa mara na watu wengine,tukiamini kuwa watu Fulani wanafikiri vizuri zaidi na kwanjia bora zaidi,wana maamuzi bora kuliko sisi au hata hatua zao ni bora na zenye maana zaidi kuliko zetu,na hivyo kujikutwa tukiwa tegemezi wa mawazo,machaguzi au hata maamuzi ya watu wengine.
Jambo la kusikitisha ni kwamba tulio wengi ni wahanga wa pingu hizo za kujilinganisha,inawezekana karibia kila mmoja wetu amewahi kujilinganisha na mtu mwingine katika nyanja mbali mbali labda shuleni,vyuoni,kwenye familia zetu,koo zetu,makazini na maeneno mengine mengi katika jamii zetu.
Inawezekana kujilinganisha kukaonekana kuwa jambo zuri tu lisilo na madhara au kama chachu ya kumfanya mtu afanye bidi zaidi ili kufikia mafanikio ambayo mtu au watu Fulani wamefikia.lakini je ni kweli kujilinganisha hakuna madhara? Je kujilinganisha ni kitu kizuri kinachoweza kumchochea mtu afanye vizuuri zaidi na apige hatua kutoka mahali alipo kwenda pengine?
Hebu tuone leo jinsi kujilinganisha kunavyoweza kutuathiri sana na kugeuka kuwa pingu zinazoweza kuathiri Ukuzi na Ustawi Wetu Katika jamii.
kwa kuanza acheni tuanze kuzungumzia jinsi kulinganisha kunavyowaathiri Watoto wetu.
Kuachilia mbali tabia, nyutu na vipawa vya kurithi,Watoto wanakua,wanastawi wanajenga utu wao kutokana na malezi wanayoyapata na jamii inayowazunguka kwa ujumla.Sasa katika heka heka za hapa na pale za malezi ya Watoto wetu si ajabu kabisa kujikuta tukiwa na tabia endelevu ya kulinganisha Watoto wetu au uwezo wa Watoto wetu na Watoto wetu wengine,Watoto wa majirani,rafiki au ndugu zetu. Si ajabu kabisa wazazi kukisika tukitoa kauli kama unamwona mwenzako X anajua kusoma na wote mko darasa moja wewe unajiuma uma tu hapa au unamwona mwenzako Y msafi kweli wewe kufua tu hata soksi zako mpaka fimbo zipite.
Kauli kama hizi za mara kwa mara zinawezaje kumwathiri mtoto katika ukuaji na utu wake?
1. Mtoto anakosa kujiamini kabisa.Sikuzote mtoto ataishia kuamini hana anachoweza kukifanya katika namna bora kama ambayo mtoto au Watoto Fulani ambao umekuwa ukiwalinganisha naye wamekuwa na uwezo wa kufanya. Hilo litapelekea mtoto au Watoto wetu kuamini katika uwezo wa wenzao na kukosa kuuamini uwezo walio nao kwa asili.
2. Mtoto anakosa kuujua ufanisi wake na kuuwekeza katika huo ili kuukuza.Zoea la kumlinganisha mtoto na mtoto mwingine linamnyima mtoto anayelinganishwa kutambua ufanisi na vipawa alivyo navyo.
Hii ni kwa sababu inamlazimu mtoto anayelinganishwa kupima uwezo wake kutokana na vipawa au uwezo wa mtoto anayelinganishwa naye huku akiua vipawa na uwezo wake taratibu kwa kuwa hakuna anayemsadia kutambua vitu hivyo, akiamini kwa kufanya sawa na yule aliyelinganiswha naye basi atakua amfenya vizuri na mzazi wake atampenda na kumfurahia.Na tukumbuke kuwa sikuzote Watoto wanahangaikia sana kupata kibali cha mzazi,kila mtoto anatamani kupenda kukubaliwa na kumfurahisha mzazi wake,hivyo Watoto walio wengi watajitahidi kufanya mengi wawezayo ili tu kuvipata vitu hivyo kutoka kwa wazazi wao. kwa nini usimchunguze mtoto wako na kujua uwezo wake na kumsaidia kuuendeleza badala ya kumlinganisha na mtoto mwingine ambaye ana vipawa na uwezo tofauti na mtoto wako?
3. Mtoto anaweza kujenga chuki kuwaelekea wale wote wanaoonekana wanaolinganishwa naye na kuonekana bora kuliko yeye.Hii ni hasa pale ambapo mtoto anajaribu sana kufikia mambo ambayo mtoto ambaye analinganishwa naye ameyafikia na anashidnwa kuyafikia mafaniko yake,na zoezi la kumlingansiah ni endelevu hivyo kujenga chuki kwa mtu anayelinganishwa naye akiamini nyeye ndiye anayependwa zaidi na ni kwa sababu yake yeye haonekani kama bora au ana msaada wowote.Hujawahi kuona mtoto akimchukia sana au dada,kaka au mdogo wake ambaye labda ana akili sana kuliko yeye,au msafi sana au labda ana fanya jambo Fulani kwa ufasaha sana?
Kama tujuavyo mtoto ndio mwanzo wa kukua kwa jamii yetua kuaniza ngazi ya mtaa,Kijiji mpaka kufikia taifa, hivyo basi tunapoendeleza tabia ya kumlinganisha mtoto wetu sikuzote tunatengeneza kizazi dhaifu kinachotokeza jamii dhaifu kwa ujumla,hata sisi leo ni mazao ya watoto ambao labda kwa namna moja au nyingine tumetokana na malezi Fulani Fulani yaliyotuathiri au labda tulikuwa waathirika wa kulinganishwa,Sasa tuone jinsi ambavyo kujilinganisha kunavyotuahtiri tukiwa watu wazima.
1. Tunakosa kujua ni katika Nyanja ipi tupo vizuri na tutie bidi hapo na hivyo kujikuta tukifeli karibia kila wakati tunapojaribu kufanya jambo Fulani.Kwa nini?kwa sababu kujilinganisha kunapelekea mtu kufanya vitu au mambo kwa kuangalia Fulani kafanya nini na amefikia wapi, kwa hiyo mara zote tutajikuta tunaiga kile ambacho wengine wamefanya kwa kuamini ni kitu bora zaidi kuliko tunachoweza kukibuni sisi na kukifanya, hivyo tutajikuta tunaishia kufanya vitu au mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kwa ufanisi na ubora unaotakiwa kwa sababu sio kitu tunachokiweza ni kitu ambacho mtu mwingine anakiweza,wakati huo huo kama tunao ufanisi wetu unazidi kupotea na kufa na wakati huo muda hautusubiri,tukija kushtuka na kulijua kosa letu wakati mwingine inakuwa ni kuchelewa sana.
2. Tunakosa kabisa kuuamini uwezo wetu. Kwa kujilinganisha tunakosa kuamini kwamba tuna uwezo wa kufanya jambo Fulani na likafanikiwa,hii ni kwa sababu mara zote tunajilinganisha na watu wengine ambao wana uwezo na vipawa tofauti na vyetu, ambao tunaamini wana uwezo mkubwa sana na wa hali ya juu,tunapofanya hivyo tunaishia kujiona sikuzote kuwa sisi hatuna uwezo wa kutimiza mambo makubwa ambayo wengine wamefanya,tunashindwa kutambua kuwa kila mmoja ana uwezo wake wa asili na vipawa vyake.
3. Tunakosa kuyaona mafanikio yetu,hii ni kwa sababu mara zote tunajilinganisha na watu wengine ambao wana tafsiri nyingine ya mafanikio na vipawa tofauti na vyetu.kwa hiyo tutakuwa hata tufanye nini au tufanikiwe vipi kamwe hatuwezi kuona kama tumefanya chochote kwa sababu tunayejilinganisha naye hajafanya mambo katika njia yetu na anatafsiri tofauti na ya kwetu ya mafanikio.
4. Tunakosa fursa ya kuishi Maisha yetu,hii ni kwa sababu mara zote tunajipima uwezo wetu,utu wetu namna yetu ya Maisha na mtu mwingine,hivyo tunajikuta kila wakati tutataka kuiga Maisha yule mtu tunayejilinganisha naye,tukiamini aina yake ya Maisha ni bora kuliko yetu.
5. Tunakosa furaha na kuishia kuvunjika moyo ,kwa sababu mwisho wa siku kujilinganisha kutatufelisha tu, hii ni kwa sbaabu kila mmoja ana vipawa na uwezo wake,hivyo hakuna njia ya kufanya kilicho bora kwa kuiga uwezo na vipawa vya mtu mwingine.Mfano mtu aliye na kipawa cha uimbaji hakuna namna atafanya bora kwa kumuiga mtu mwenye kipawa cha uigizaji,kwa hiyo tukilazimisha maanake ni lazima tu tutashindwa na matokeo yake ni kuvunjika moyo kwa kushindwa mara zote.
6. Tunaishia kujiumiza na kutumia nguvu nyingi sana zisizo za lazima ili tu kujithibitsha kuwa sisi ni bora kuliko wengine.Hii hupelekea hata ufanisi wetu wa kazi zetu au biashara zetu kuwa mbovu kabisa,kwa sababu badala ya kufanya kazi zetu kwa bidii kufikia malengo yetu tunaishia kufanya kazi kwa bidi ili kuthibisha kwamba sisi ni bora kuliko X,matokeo yake ni kwamba utendaji wa kazi wa aina hii haujawahi kufanikiwa hata mara moja,kamwe usifanye kitu kwa ajili ya kutaka kuthibisha kuwa wewe ni bora kuliko mtu mwingine,fanya kulingana na uwezo wako.
Baada ya kuona hayo basi, tufanye nini kuhusu kujilinganisha ?
1. Tukumbuke kuwa kila mwanadamu ameumbwa kwa njia ya pekee na hakuna ambaye anaweza kulingana kabisa na mtu mwingine.tukilijua hilo hatutashawishika kujilinganisha kivyovyote vile na mtu mwingine tutajizingatia sisi kama sisi na kuwezekeza katika kujifahamu vizuri na kufanya kazi kulingana na jinsi tulivyo na vipawa vyetu.
2. Hata tuwe na vipawa vingi kadiri gani,tuwe na utu wenye nguvu kadiri gani sikuzote kutakuwa na mtu aliyetuzidi kwa namna moja au nyingine ,hii ni kanuni ya Maisha ambayo ipo sikuzote,popote pale unapokwenda,na ipo hivyo.hata uwe na mke au mume mzuri kama malaika ,lazima kuna mtu amekuzidi mahali Fulani huko,hata uwe mrembo au kijana mwenye mvuto wa aina yake lazima kuna mtu mahali Fulani amekuzidi huo urembo na utanashati wako.Hivyo basi tukilijua hilo na kuliweka akilini hatutakaa tujilinganishe na wengine tukijua kuwa lazima kuna wengine walio na uwezo na vipawa tofauti kabisa na vyetu na watafanya vizuri zaidi kuliko sisi.
3. Tukumbuke vizuri Maisha ni Kutegemezana sikuzote, ili Maisha yaende ni lazima kila mmoja afanye sehemu yake,kila mwanadamu anahitajika kwa namna yake ya pekee ili Maisha yaende nay awe yenye furaha,fikiria sisi sote tukiwa madaktari,nani awe hakimu,nani awe mjenzi na nani awe mkulima? Au kama wote tutakuwa wasemaji wazuri,nani awe msikilizaji? Nani awe kiongozi?nani awe mtekelezaji? Tukilifahamu hilo hatutasumbuka kujilinganisha ila tuatafanya yote tuwezayo kutumia vipawa vyetu ili kuiboresha jamii kwa kadriri ya vipawa na uwezo wetu unavyoturuhusu.
4. Kama tulivyoona huko juu,familia ni kianzilishi cha jamii,hivyo basi tukiwa kama wazazi tuijtahidi sana kuwalea Watoto wetu kwa kuzingatia uwezo na vipawa vyao badala ya kuwalinganisha mara zote na Watoto wengine.Tuwekeze katika kukuza vipawa na uwezo wao. Hii itatokeza kizazi bora chenye furaha ,kuridhika na kufanya kazi kwa bidi ili kuleta maendeleo yenye tija katika jamii yetu kwa kutumia vipawa na uwezo wao vya asili ipasavyo.
Mwishowe namalizia kwa kusema tena tujitahidi kujiondoa kwenye pingu za kujilinganisha ,tuwe huru kutokana nazo ili tuiboreshe jamii yetu,tupate watu wenye ufanisi kutokana na vipawa na uwezo wao wa asili.Tutumie vipawa na uwezo wetu kuiboresha jamii badala ya kufikiria namna ya kufanya mambo kama uwezo au vipawa vya watu wengine.
Asanteni.

Upvote
4