Mohammedy Al Hajji
Member
- Jul 17, 2016
- 6
- 3
Thamani ni Chakula, fedha ni namba huna uhakika nazo.
Utajiri ni chakula, Walioamua kulima wakisema hawauzi chakula chao, sijui kama tutaweza kula hela. Chakula ndio utajiri kwa kuwa ni mfumo asilia wa kimungu.
Hela sio utajiri hela ni mfumo wa namba ulioanzishwa na wasiokuwa na mali. Walipoona hawana thamani nyengine kwenye mikono yao, ikabidi watafute mfumo ambao utawafanya waishi. Wakausambaza ulimwenguni kwa njia zenye sura mbili tofauti. Walitumia sura ya kutisha kwa kutumia silaha na walitumia sura ya huruma kwa kutumia dini.
Haya yote yalivunja ukuu wa mtu mweusi na kumfanya mtu mweusi kuwa mtumwa. Anabeba asiyoyajua kwa maana ameambiwa "mungu anajua yote na atakutendea. Na kwa hilo mtu mweusi anaogopa." kila mtu leo anapambania hela ili anufaishe tumbo jambo ambalo linamfanya mtu mweusi asiwazie tena wengine kwa kuwa anaona kuimarisha tumbo lake ni vyena zaidi ya wengine. Tamaa za fedha na mali zimemfanya mtu mweusi leo kuwauza ndugu zake, hawezi kuyasema yaliyo gizani kwa kuwa anahisi yeye ni bora kuliko wengine.
Ubinafsi wa kujiona wewe ndio bora kuliko wengine ndo kunasababisha waumini wawahukumu walio nje ya dini kwa kuwaona ni waliopotoka, ndo kunasababisha wasomi wawaone wasiokuwa na vyeti kuwa ni waliokosa maarifa. Ndo kunasababisha viongozi wa serikali kujiona wao wapo sahihi kwenye lolote wanaloamua kulipanga. Watu weusi hawaaminiani tena kwa kuwa wanauza ndugu zao ili wapate wasichokuwa na uhakika nacho.
Zamani watu waliungana wakalima pamoja, walisaidiana kwenye mambo mengi pamoja na kwamba hawakuhubiliwa dini wala kupewa mawaidha. Leo hatusaidiani japo ndio tunaoongoza kupishana kwenye nyumba za ibada. Epuka kuwatenga ndugu zako kwa kimvuli chochote kile chenye nyanja za ubaguzi. Epuka kumuuza mtu mweusi.

Upvote
0