Kujisajili crdb katika simu

Jewel

Senior Member
Joined
May 1, 2008
Posts
180
Reaction score
65
Jana nimepata taarifa kwamba unaweza kujisajili atm card ya crdb katika simu yako. Nauna uwezo wa kutuma na kupokea pesa hata kuamishia tigo pesa,je hii ipo safe siwezi kubiwa na mtu kwa kutumia simu yake? Au mpaka apate simu yangu ? Naomba shauri
 
CRDB usijaribu, mi nimepatiwa Tembo Mastercard yao lakini kila siku salio langu linapungua. Nikiangalia kwenye benki statement naona Description ya transaction ni POS txn ....sasa sijui hawa jamaa siku nikiwaibukia watanieleza nini.
 
It is risky is if someone else knows your PIN code, or if you think you could loose your PIN code to untrusted party.
Other than than, I don't see the risk.

However, I wouldn't so much trust something that involves tiGo. This is a very subjective opinion though, be warned. I don't have any solid reason, but personally I can't entrust very sensitive information to tigo after all the drama I have heard about tigo pesa.

I use this service but with Vodacom.
 
Is the service applicable to tigo pesa only? What about m-pesa( voda )?
Otherwise I don't see the problem with the service as long as you will keep your details personal.
 
iam technophobic,anything involves e banking is dangerous.
 
Jamani anayejua jinsi ya kujiunga na hiyo huduma ya Crdb mobile anijulishe mie nataka kujiunga sasa hivi.
 
Hiyo mpaka uende kwenye tawi lao lililo karibu yako, wao watakuombea azikiwe.
But kama uko dsm waweza kwenda azikiwe branch utaelekezwa floor ya ngapi sijui pale ghorofani
 
Jamani anayejua jinsi ya kujiunga na hiyo huduma ya Crdb mobile anijulishe mie nataka kujiunga sasa hivi.

Wakuu,hii huduma ni nzuri,waweza toa pesa toka CRDB kwenda
1.mpesa, zap
2.account zako nyingine.
Pia waweza
1.jua salio
2.kujua statement fupi,na mihamala mingine
risk ipo kwenye kutunza password.
JINSI YA KUJIUNGA:tumia line ya vosta(mostly)kujiunga au airtel,tigo wazushi,piga *150*03#
baada ya hapo process ni zile kama za mpesa au tigo pesa we fuata maelezo tu zingatia.vifuatavyovitahitajika kuingiza ili kujisajili
1.andika pembeni namba ya kadi ya ATM(ile namba ina matarakimu mengi).
2.andaa namba yako ya account.
3.andaa namba yako ya siri unayoitumia kwenye atm,hii itajitajika ili kugenerate password mpya.
4.andaa four digit password mpya(hii utaitumia kulog kwenye sim banking yako).

Hope ni hayo tu wakuu kwa ufafanuzi usisite u will enjoy.pia kwa internet banking nenda kwenye tawi umefungua ac yako ujaze fomu ili upate internet banking
NAWASILISHA.
 

Mbona nimejaribu line ya Voda imekataa?
 
Jamani kwa sisi wa NBC Kuna huduma kama hiyo? Kama ipo anayefahamu atueleze.
 
nimejaribu kuijisajiili lakini date format ndio inanisumbua, unatakiwa uingize expiry date ya card, kila nikiingiza inakataa, format ya expiry date inatakiwa iweje?
 
CRDB mpaka uende katika branch uliyofungulia akaunti ujaze form ya application ant terms agreement then wanakutumia set up file
(you must have a phone with internet capability) unaaccept na kuinstall hiyo application ktk cmu yako then you can start using it! NOTE: usijazejaze inf zako online utakombwa akiba yako!
 
nimejaribu kuijisajiili lakini date format ndio inanisumbua, unatakiwa uingize expiry date ya card, kila nikiingiza inakataa, format ya expiry date inatakiwa iweje?

mkuu hapo ni kwamba,kama inaexpire mwezi wa tatu 2011 unaandika 0311,hakuna space wala chochote unaacha,kama ni december 2012 ni hivi,1212 jaribu mkuu hiyo.
 
Gharama/makato/charges kwa huduma hii ni shilingi ngapi?Koz mi sijafanya research ila naamini crdb ndio wezi wasio na mfano hasa when it comes to service charges...mfano kwny atm huwa nashindwa kuelewa wanavyokatakata hela unaona tu elfu tano tano zinakatwa ovyo ovyo..sjui kwa hii huduma ikoje anayefahamu atujuze plz
 
Mkuu hii huduma ya simu banking crdb hawaiwezi! mana they are very poor in handling customer complaints, and follow up of hick ups.

Na kwa uzubaifu wa Bank Kuu na TCRA basi wateja ndo wanaumina.

case in point.
Jumamosi Tar 14/09 nimehamisha pesa toka account yangu ya crdb kwenda kwa namba yangu ya simu ( MPESA)
Hiyo transaction haijawa effected toka Jumamosi Tar 14/09 saa 4 asubuhi, hadi leo J'tatu tar 16/09 saa 10 jioni, pesa imetoka kwenye account ya benki, lakini kwenye Mpesa haikuingia na wao wameekaa kimya tuu.

Kuuliza Branch - Tower branch, - Dada anaitwa pale maulizo anaitwa Tunu, ni kichefuchefu! hajui hata la kufanya naona amekaa tu kama anasubiria tunu.

Kupiga simu customer service ndo kabisaa! eti "tunashughulikia"!!

Hawajuai kuwa nini maana ya mtu kuweka pesa kwenye current account! - unatakiwa kumpatia pesa yake anytime akiitaka bila usimbufu!! mama anaweza kuwa na mgonjwa sasa J'mosi hadi leo J'3 mgonjwa hajafa??
 


..Mkuu, Hii inayozungumzia ni ile ya INTERNET BANKING ambayo ni lazima simu yako iwe na uwezo wa Internet na lazima ufike kwenye tawi lako kujaza form lakini kuna hii ya *150*03# wanayoiita SIM BANKING kama sikosei ambayo unaweza kujisajili mwenyewe kwenye simu yako hata ukiwa nyumbani tu na si lazima simu yako iwe na uwezo wa Internet.

 

Mkuu, hata mimi hii iliwahi kunipata. Nilihamisha pesa kutoka akaunti yangu kwenda Mpesa kwa kupitia SIM BANKING Jumamoji saa 12 jioni fedha ikaja kuingia kesho yake Jumapili saa Tano asubuhi baada ya kupigishana sana kelele na Watu wa Huduma kwa wateja. Lakini niseme tu kuwa Most of the Time, Huduma hii ni njema pamoja na hizo Hiccups za hapa na pale.
 
Unaweza kusajiri ukiwa nyumbani kwako, ila mtu mmoja wa crdb alinidokeza kuwa,kutoa hela crdb kwenda m-pesa kwa line za voda ni rahisi zaidi kuliko line ya Airtel. Ni kweli, nilijaribu sana kwa line ya airtel, ni ngumu. Pili huduma hii nimeipenda hasa kwa kupunguza muda unaopotea ktk foleni barabarani na benki kwenyewe na kuongeza usalama, hasa unapokuwa unataka kubeba hela nyingi kumpa mwenzio mwenye ac crdb. Crdb hawana maximum ktk kuhamisha within crdb bank, tofauti na Nmb ambao kwa siku mwisho laki tano.

Mapungufu yapo, lakini kwa sasa, SIM BANKING inaokoa sana muda na kuongeza usalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…