Kujiua/Kujinyonga ni ubinafsi na kuwaachia shida zako watu unaowaacha

Kujiua/Kujinyonga ni ubinafsi na kuwaachia shida zako watu unaowaacha

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Anaandika Ndugu MalisaGJ
TATIZO LA KUJIUA KATIKA JAMII

"Kwako mke wangu
(Mama Derick). Naomba nisamehe sana kwa maamuzi haya. Maisha kwangu hayana maana tena, nisamehe sana. Nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze watoto wetu” sms ya mwisho ambayo Sajenti William Giriango Chacha (40) askari wa JWTZ alituma kwa mkewe, dakika chache kabla ya kujinyonga kwa mkanda wa suruali huko Dodoma.

#MyTake:
1. Tatizo la afya ya akili ni kubwa sana kwenye jamii zetu kuliko tunavyofikiri. Kuna haja ya serikali, wadau mbalimbali (NGOs) na jamii kwa ujumla kuchukua hatua za makusudi za kukabiliana na tatizo hili.

2. Ukipata tatizo hata liwe kubwa kiasi gani jitahidi kuzingumza, usikae kimya. Kuzungumza kunapunguza risk ya kufanya maamuzi mabaya ikiwemo kujidhuru.

3. Hakuna binadamu ambaye ni bingwa wa matatizo. Uwe tajiri, maskini, mnene, mwembamba shida haichagui. Hakuna watu majasiri kama wanajeshi. Lakini pamoja na ujasiri wake, Sajenti Chacha ameshindwa kuonesha ujasiri huo kwenye matatizo, hatimaye ameruhusu matatizo yamshinde.

4. Kujiua kwa sababu ya matatizo ni kuwaachia matatizo makubwa zaidi uliowaacha. Mke na watoto wa Chacha wanaenda kukabiliana na changamoto nyingi za maisha baada ya baba yao kujiua, kuliko changamoto walizokua nazo baba yao akiwa hai.

5. Kama unaipenda familia yako, mkeo, watoto, na ndugu zako, usijiue. Kujiua ni ubinafsi. Kujiua ni njia rahisi ya kumaliza matatizo yako lakini kuacha matatizo makubwa zaidi kwa ndugu zako na marafiki. Kujiua ni kuacha alama ya maumivu isiyofutika kwa familia yako.

6. Matatizo yakikuzidi hakikisha huwi peke yako. Hakikisha unaye wa kumwambia hata kama una uhakika hawezi kukusaidia, we mwambie tu. Kushare matatizo yako ni sehemu ya healing process. Ni psychosocial therapy.
 
Kujinyonga huwa naona ni kazi ngumu kuvumilia zaidi ya ugumu wa maisha, watu wanaojinyonga kiuhalisia ndio wanatakiwa wawe wapambanaji zaidi ya wengine, lakini nashangaa, wale makamanda wa kutuongoza vitani ndio huwa wa kwanza kukata tamaa.

Tunatakiwa kuwa wavumilivu sana na haya maisha, ni magumu kwa wote labda kasoro wale wanaotafuna tozo zetu, linapokujia wazo baya kichwani, jitahidi uwezavyo kuliondoa akilini haraka kabla halijakuteka uanze kufikiria namna utakavyolitekeleza.

Ishi maisha yako kama yalivyo, jikubali, wapende wanaokuzunguka, amini iko siko hali yako itabadilika, tafuta tabasamu lako toka kwa watu wako wa karibu; watoto, mke, au mume, ndugu na marafiki, kamwe usijilinganishe na mwingine, hayo mawazo mabaya huwa ni kama upepo tu, baada ya muda hupita.
 
Unajinyonga na bei za mbao hazishikiki, at least ukitaka kujiua uache pesa ya jeneza.

Point : ni muhimu kusikiliza, kushauri na kusaidia mtu anapokuwa kwenye shida
 
kaka bujibuji anaejiua huyo no mwanaume kwelikweli, ukiwa na roho ya kike huwezi jiua au nasema uongo ndugu zangu
 
Badala ya kujinyonga,badili laini ya simu potelea mikoa ya pembezoni huko utarudi uzeeni
 
Suala la afya akili linatakiwa liangaliwe kwa jicho la tatu ,matukio mengi ya kujiua na kuua yanatokana na watu kutokuwa serious na wanayokutana nayo, always kama utaruhusu kila jambo au tukio kukupanda kichwani ujuwe unajichimbia kaburi la kujizika mwenyewe,madhara yanakuwa makubwa kuliko yule anayeua au kujiua kuyatambua, huyohuyo kuna watu wanamtegemea.

Suala la kuzingatia ni kuwa pindi upatapo changamoto suluhisho ni kumtafuta yule unayemuamini ,umlezee shida zako ,huenda sentensi moja itayo toka mdomo mwake ikabadilisha twasira nzima ya Yale unayoyafikiria.

Jambo jingine ni kuwa wengi wetu wakikutana na changamoto wanatumia muda mrefu kuifikiria changamoto ile,jambo linalotufanya some times kufanya poor decision making, wengi wetu huwaga tunafikiria matendo hasi badala ya chanya, bora udhalilike lakini ufanikiwe kuitatua changamoto yako na maisha yaendelee ,utakapo jiua kile uichokuwa unakificha watu watakijua .

Embu jiulize utakapo jiua utaenda kumjibu nini Mungu wako, nakijiua ni tendo la kiiisheitwani, lakukumbuka unatakiwe usiwaaamini sana watu kikulacho kinguoni mwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom