Kujiuzulu kwa Mbeki, Je ni ufisadi ulioshinda?

Kujiuzulu kwa Mbeki, Je ni ufisadi ulioshinda?

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,081
Reaction score
2,325
Taarifa za kujiuzulu kwa Mbeki zimekuja kama gharika. Viongozi waliosababisha Mbeki ajiuzulu uraisi wanajulikana. Wana kila tuhuma za ufisadi huko kwao. Wote tunajua jinsi Zuma alivyokuwa na tuhuma ambazo kimsingi haziwezi kudhibitishwa mahakamani. Ili kujinasua na dhahama ya kupelekwa mahakamani aliamua kutumia fimbo ya kisiasa kujiokoa. Ameweza. Jambo moja la kujua ni kuwa watu wa aina ya Zuma ni wataalaamu wa mbinu mbalimbali za kuhakikisha hawaanguki. Ni king makers, waongeaji wazuri mno, wanavuta hisia za watu na kadhalika. Sijamsikia Mbeki akituhumiwa na kashfa ya kifisadi, labda kwa kuwa alikuwa Rais. Tusubiri labda atatuhumiwa.
Lakini kilichomuangusha Mbeki ni ufisadi wa wenzake wakiobaki madarakani. ufisadi aliotaka kuhakikisha unakomeshwa.
Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom