Kujiweka low profile kulivonikosesha mchumba!

Kujiweka low profile kulivonikosesha mchumba!

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Aseeh wakuu wanajf people's powers lakini pia kazi iendelee!

Katika Harakati za Kila siku bhana nikaamua kuwa navaa kawaida na nguo za bei cheeeh! "ilikuja haswa Baada ya kuwa navaa smart sana nikipita sehemu Nikitaka Ata nikabargain bei naambiwa" kaka" kwa mwonekano wako wewe huwezi kosa fedha ya kununua vitu kama hivi!

Sometime nikivaa smart sana nikapita aidha baa au karibu na majirani wanaonijua Baada ya dakika kadhaa vizinga vingi wakihisi nimeshajipata🤣kumbe napenda kuwa nadhifu tu

Basi! Nikakumbuka mwanangu alinambia "oya mwanangu uwe unavaa ki-lowkey mzee ujue nani ni mtu wako wa kweli🤔😂

Bas si mjuba kwa fuasi nikachekecha mavazi fulani ya kilocal, sasa mida ya jion nikiwa natoka hussle nikakutana na mdada Ile kumuongelesha tu akawah kuficha pochi lake kwapani(moja kwa moja nikajua haya mavazi yangu yameuogopesha) yule demu akanichomolea

Siku nyingine nimevaa kikawaida sana, nikaingia kwa wakala mmoja wa mitandao kutoa hela nikashangaa anawachangamkia mabraza waliovaa smart mimi nilievaa kilocal akanisuburisha

Siku ingine nimeenda Cafe moja hiv nzuri tu nimevaa hivo hivo kawaida nikashangaa wahudumu hawanizangatii, wanawazingatia wale walionyuka pamba!

One time Tena nikaenda ofisi moja hivi nimevaa tu shat yangu na suru.. kitambaa, wakaingia mabraza wamenyuka vyuti,Tai, kiatu embe sindano😂nkaona kama napuuzwa,ila mavazi yangu was the point

But popote nilipokua navaa kwa kupania(mwonekano mzuri) huduma nilikua napata fasta na bebezi nazikoa Ile ile hazikabi

Mimi sikubaliani na watu wanaosema jiweke kawaida uone nani atakuthamini, kimsingi ukiwa nazo pesa nyuka pamba, tembea na chuma kali, (ila usikope kuwatambia watu utakufa vibaya😂

Haiwezekani mtu ukoswe hela na mikwara ukwose! 🤣Haiwezekani Kila angle uwe mnyonge
 
Low profile au low key haipo hivyo Kama unavyoandika hapa.

Ulichokuwa unafanya wewe sio low profile au low key Ila ni commoner yaani unavaa na kuishi Kama MTU wa kawaida.

Ila low profile -ni Kama unavyomuona Mgwana samatta

Kuwa low profile na kuwa commoner ni tofauti kabisa

Lugha nyingine ya low profile ni humbleness .

So akichoandika Robert Heriel Mtibeli haukumuelewa
 
una miaka mingapi??maana siku ukikua utaelewa kwamba kinachokutanisha watu ni utu wenu sio viambatanisho vyenu.
ukipendwa au kukaribiwa sababu ya nguo,gari,kazi,simu,cheo kaa kimkakati hujafatwa wewe hapo.

hasa mwanamke ndio kabisaa usifanye hilo kosa la kumshawishi kwa vitu,fanya uwezavyo akupokee kirundu kama kirundu ulivyo,ucheshi wako,ukauzu wako,uchangamfu wako,ukarimu wako nk maana hivyo vitu huyo ndio wewe.hutabadilika.
 
[QUOTE="Philomena3, post: 51722290,

Mimi sikubaliani na watu wanaosema jiweke kawaida uone nani atakuthamini, kimsingi ukiwa nazo pesa nyuka pamba, tembea na chuma kali
[/QUOTE] Umezunguuuuuka hili ndo ukilotaka kulisema.
 
Back
Top Bottom