Kujuana na watu wengi(Networks)!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,158
Reaction score
4,449
Wadau mwenzenu nimejaaliwa kuwa na marafiki wengi sana ukiachilia mbali wale niliofahamiana nao katika maisha ya shule na nika-maintain urafiki nao, lakini bado katika mazingira ya kazi na maisha ya mtaani napendelea sana ku “keep in touch” na watu wengi sana ambao nakutana nao. Kama mjuavyo watu wengi maisha huanza kwa kuwa wapangaji, hapa Dar maisha nilianzia Manzese nilikaa mwaka mmoja na nikajikuta nina marafiki kibao, nikahamia Sinza nikapata marafiki kibao, Nikahamia Tabata nikajipatia marafiki kibao, nikahamia Mbezi Tank Bovu nikajipatia marafiki pia, na mwisho nipo Tegeta nako nimepata marafiki wapya wengi tuu na kama kawaida huwa na “keep in touch” Miaka yoote nimekuwa nafanya hivyo kwa makusudi kabisa kwasababu nimekuwa nikisikia kwamba kujuana na watu wengi(Networks) ni kitu muhimu sana.


Mpaka sasa sijajua umuhimu wa kujuana na watu wengi zaidi ya Usumbufu, kwa mfano hapa nilipo nina kadi kumi na nane 18 za michango ya Harusi, Send offs, Vipaimara, Anniversaries nk. Haishii hapo nina SMS Tatu zinaniomba nihudhulie hizi weekend mbili bila kukosa vikao vya kwanza vya Harusi na Sendoffs.


Kujuana na watu wengi kumenifanya ghalama zangu za kuishi ziwe kubwa sana. Nifanye nini ili uwingi wa marafiki zangu na mimi uninufaishe???
 
Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe

La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa
 
Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe

La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa

Yaani inanitesa sana nimelileta hapa kwasababu kuna jamaa mmoja alikuwa mpangaji mwenzangu kule manzese miezi mitatu iliyopita alikuwa mmoja kati ya watu ambao nilikacha kumchangia, lakini amenielewa vibaya sana kwamba sasa hivi mambo yangu yamekuwa vizuri wao nimeamua kuwatupa maana siyo watu muhimu tena kwangu, imeniuma sana!!!
 
Najua watu wa kutosha na sijawahi kuchangia sijui harusi na vipaimara. Kama mtu anataka kufanya sherehe kubwa ajitegemee.
 
Network ni muhimu sana.
Kama mambo mengine yalivyo yana faida na hasara zake.
Lazima ujifunze kubalansi hivyo vitu.

Hasa ungekuwa unatumia hizo network kwenye kutafuta opportunities kwa ajili ya kukua hasa katika mambo ya kazi na biashara.
Hata kijamii umekua kwa kujuana na watu wengi nadhani.
 
izo story za kuchangiana mnazipenda wenyewe,wanakuletea hizo kadi coz wanajua lazima utachanga.mi nawashangaaga kweli ivi unavyolalamika kwani wanakuforce?apo ungeombwa harambee ya kurekebisha kanisa au msikiti usingetoa lakini sherehe mnapenda kweeeli yaani.wabongo bana
 
mmh chagua ndugu unazoona za maana changia zingine piga chini sio lazima ww 2 uchangie kote uko jaman.
 
Kadi za harusi? We acha tu! Kuna wakati zilinisababishia headache mpaka nikachanganyikiwa. Ikafika kipindi nikaweka mkakati kuwa hata nipewe kadi kumi, nitachangia kadi mbili tu kulingana na closeness na wahusika. Zinazobaki kapuni.
Vikao vya harusi? Huwa inategemea kama nina nafasi au la. Otherwise, napiga chini. Unajua jumapili mara nyingi ndiyo huwa muda wa kupumzika hivyo hakuna haja ya kubeba majukumu mengine ukajikuta unaenda kazini jumatatu ukiwa hoi.
Tusielewane vibaya jamani, lakini haya mambo tunapoelekea yatarudi kuwa ya kifamilia kama ilivyokuwa zamani!
 
Kujuana na watu wengi ni faida kubwa ila ukiangalia faida ya kitu utaona hakuna maana!napili kuna mkundi yakujuana hivyo unaweza kuwa na kundi la marafiki lakini ukiwa na shida ya ukweli hakuna rafiki hivyo yakupasa uwe mwangarifu sana na marafiki!!mimi binafsi napenda marafiki lakini marafiki wangu ni wale wakutoa ushahuri siyo wakuwalilia shida!Mfano unaenda baa umekunya pombe zako mara polisi wamekuja wanamtafuta mtu kaua kakimbia lakini mavazi ya huyo aliyekimbia nikama yako wanakuchukua na wanasema niwewe jambazi uliye ua kwa bunduki&na wanataka hiyo smg wewe unasema siyo mimi jamani wanasema niwewe!je katika marafiki zako wote kuna mtu anaweza akapiga simu kuongea na Kova,au IGP,Vua Naodha,au watu wa sampuli hiyo?kama unao basi hao ndo marafiki wako na wakuwaintateini.
 
Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe

La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa

Pole sana bro ndio wabongo walivyo.

Wengine watakutafuta kama deni.

We uchangie usichangie harusi itafanyika
 
Najua watu wa kutosha na sijawahi kuchangia sijui harusi na vipaimara. Kama mtu anataka kufanya sherehe kubwa ajitegemee.

Lakini ndiyo mwanzo wa kuwapoteza
 

Kumbuka kama umepewa kadi kumi ukachangia mbili tuu hizo nane umetengeneza watu nane wa kukukasirikia kisaikolojia tayari umeleta tatizo moyoni
 
Lakini ndiyo mwanzo wa kuwapoteza

Niwapoteze kwasababu sichangii vitu ambavyo sio vya msingi? Acha niwapoteze tu. Kama wana shida, ugonjwa, hawana chakula naweza hata nikakopa kwaajili yao ila mambo ya harusi hapana. Kwanini mimi nigharamie sifa za mtu mwingine?
 

Kwenye hili la michango, kama kwa namna moja ama nyingine hii network yako ilikuchangia (say katika harusi etc), then unao wajibu wa kurudisha fadhila. Au hata kama unategemea na wewe kuja kuwachangisha kama ukipata "shughuli", then ni vema 'ukawekeza' kwao (ingawa niseme pia kwa uangalifu!).

Hasa katika kipindi hiki cha taarifa ("information age"), network kwa ujumla zinasaidia sana hasa kama umeweza kutengeneza network ambayo ipo diversified vya kutosha kwa maana ya ujuzi, jinsia, social status, na hata vipato (sio kama wewe fundi engineer basi network yakop yote ni maengineer tu!). Lakini pamoja na kusaidia huko hapahapo kuna mtego pia...kwamba na wewe lazima usaidie wengine. Cha muhimu tu ni vema kwa kadiri unavyoweza kuweka mipaka ya kiwango na aina ya misaada(information) mnazoweza kusaidiana/kupeana.
 

Ina click
 
Niwapoteze kwasababu sichangii vitu ambavyo sio vya msingi? Acha niwapoteze tu. Kama wana shida, ugonjwa, hawana chakula naweza hata nikakopa kwaajili yao ila mambo ya harusi hapana. Kwanini mimi nigharamie sifa za mtu mwingine?
Kwasababu ni rafiki yako!!!
 
Usiishi kwa kufurahisha watu ishi vile wewe utakavyo. Utapokuwa unaenda kuchangia nambie namie niwatume TRA waje wakusanye mapato yao.
 
Kuna tofauti ya kujuana na rafiki. Rafiki ni Yule anayeweza kuwa nawe wakati wa dhiki, kujuana ni Yule anayekujua na si lazima awepo wakati wa dhiki ila Mara nyingi Yuko wakati wa raha.

Fanya kile unachotaka. Michango ya harusi, kipaimara ni matumizi mabovu ya hela hivyo Probability ya kupata ni karibu na Zero hata kwa familia yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…