tujuemoja
Member
- Jul 26, 2022
- 7
- 2
Katika Kutatua Changamoto Mbalimbali za maisha kuongea na kunyamaza ni njia ambazo zimekuwa Zikitumiwa na Watu.
Ingawa Watu wengi Wamekuwa na dhana potofu ya kwamba kukaa kimya kwa wakati wote ni sahihi Sana kuliko kuongea. Jambo linalopelekea waongeaji kuonekana watu wasio na staha katika jamii yetu.
Hekima na busara kamwe haiwezi thibitishwa katika Mambo mawili tu (kukaa kimya au Kuongea). Bali inategemeana na Matumizi Sahihi ya Ukimya au Uongeaji.
Vitabu Vya Dini Vinasema kwamba, "Wakati wakunyamaza na wakati wa kunena" Mhubiri 3:7
Nimefanya tafiti katika Suala zima la kukaa kimya au Kuongea katika jamii yangu ya chuoni. Kwa kuuliza jamii yangu Swali Lifuatalo "JE KUKAA KIMYA WAKATI WOTE NI SAHIHI SANA KULIKO KUONGEA"
Mawazo yao katika kukaa kimya au kuongea yalikuwa kama ifuatavyo:-
MWANACHUO WA KWANZA:-
"Ni sahihi kukaa kimya wakati wote kuliko kuongea lakini kuna mazingira yanayotufanya tuongee ila katika kuongea inatakiwa ulimi uwe na uhusiano na ubongo".
MWANACHUO WA PILI:-
"Si sahihi kukaa kimya wakati wote
Bali kuna nyakati unapaswa kukaa kimya ila kuna nyakati unapaswa kuongea"
MWANACHUO WA TATU:-
"Kila kitu kina kiasi chake kwa hiyo sio kila wakati wa kukaa kimya na sio kila wakati wa kuongea"
MWANACHUO WA NNE:-
"Kukaa kimya sio suluhu ya mambo kuna wakati utakaa kimya na kuna wakati utatakiwa kuzungumza lakin katika kuzungumza inahitajika hekima na busara Kwa kilaa neno utakalolitoa. " Kuwa taswira ambayo ni fumbo kwao"
MWANACHUO WA TANO:-
"Ni sahihi hasa ingawa sio sana kukaa kimya.Binafsi huwa ninaamua niko wapi na je! nizungumze! au nisikilize.
Wanaokaa kimya kwa muda mrefu wamebainishwa na wengi(Watu)kama wastaarabu au wapole wakati wengine wanaokaa kimya ni kinyume chake.
NB:Ni nafuu kukaa kimya.
Hayo ni baadhi ya Maoni ya wanachuo kulingana na Swala zima la kukaa kimya au Kuongea.
Hitimisho langu katika Tafiti hii Nilihitimisha kwa kubaini vitu kaadhaa ambavyo wachangiaji walitoa mawazo na mitazamo yao, Kwanza Hakukua na Mchangiaji aliyeungana na hoja kwa asilimia zote, Hii ni kwa sababu ya Matumizi ya maneno(ila, lakini, sio nk) yaliyoonyesha kuwa na wasiwasi kukubali upande mmoja wapo wa kukaa kimya au Kuongea.
Kitu Cha pili, Niligundua wachangiaji waliweza kuelezea vitu vya msingi katika kuchagua kukaa kimya au Kuongea.
Na mambo hayo ni kama yafuatayo:-
01. Nyakati/wakati/Muda
Katika kuzungumza au kuchagua kukaa kimya ni muhimu kuzingatia wakati uliopo kama ni sahihi wewe kukaa kimya au kuzungumza.
Mfano wa Nyakati za Ukimya:-"Wakati wa kupewa maelekezo ni vizuri sana kukaa kimya mkapa mwisho wa maelekezo hili kuepuka mgongano,na kupishana na Maelekezo ".
Mfano wa Nyakati za Mazungumzo :-Waswahili usema, "Asiye uliza, Aambiwi Maana".
Hivyo basi kuna Nyakati ambazo unapaswa kuuliza kwa sababu ya kushindwa kuelewa ulichoambiwa.
02. Mazingira
Katika jamii zetu kuna maeneo ambayo yamepigwa marufuku kwa mazungumzo ya kelele mfano, Hospitalini nk.
Hivyo basi unapaswa kuzui mdomo wako kuzungumza ili usije ukaleta madhara yatokanayo na onyo hilo.
Pia, Maeneo ya Kama Michezoni ni ajabu kumkuta Mtu aliyeenda kwa dhumuni la kushangilia kafumba mdomo uwanjani labda kama upande wake umeshindwa. Hivyo basi ruhusu mazingira kukuamrisha kuzungumza.
03. Kiasi.
Ni moja ya vitu vya msingi sana ambavyo inapaswa kukuongoza kukaa kimya au kuongea. Mara zote ninapenda kusema kuwa, "Kizuri Usilewe kwacho, Nipe Kiasi Nafasi".
Kanuni hii inatumika katika sehemu zote hata haijalishi umeongozwa na wakati au mazingira nk.
04. Uhusiano baina yenu.
Kuna Nyakati ambao unafika katika hali ambao mazingira, nyakati na kiasi Zimekupa ruhusa za kuzungumza lakini kwa sababu ya uhusiano baina yenu yanataka usingumze, Uenda ni kwa sababu mnahusiana katika kazi, mzazi, rafiki, jirani n.k
Ni kipengele ambacho hekima na busara hufanya maamuzi ya kutambua uhusiano wa uliopo katika yako na mzungumzaji mwingine.
05. Nidhamu.
Kuna Nyakati kukaa kimya ni nidhamu na inaweza isiwe nidhamu kwa upande mwingine. Hivyo basi nidhamu yako inatambulika kwa maamuzi utakayofanya kwa wakati usika kwa kukaa kimya au kuongea.
Mfano:-Nidhamu ya Kuwinda ni kuwinda bila kelele, Kelele havipelekane na uwindaji hata siku moja, Kwa kufanya hivyo inakupa sifa ya wewe kupata unachowinda.
Hivyo basi ufanyapo uamuzi wa kukaa kimya au kuongea unapaswa kuzingatia hivyo vitu vitano hapo juu.
KUMBUKA:-"Ukikutana na Mtu anayefahamu Mambo Mengi Kuliko wewe Nyamaza kuwa mpenzi msikilizaji na muulizaji"
Na hii ni kwa sababu utakuwa ukizungumza kitu kilekile unachokifahamu kwa kujirudiarudia bila ya kujifunza jambo jipya katika akili yako. Na hii ni hatari sana. Lakini kwa kukaa kimya uzalisha fikra ya kufikiri jambo kwa kina na kwa kuuliza upanua udadisi na uelewa katika jambo hilo.
MWISHO: Matamanio yangu ni kwamba tafiti yangu niliyoifanya imesaidia jamii kuondokana na dhana potofu kuhusu "waongeaji ni watu wasio na staha na wasio wa ongeaji ni watu wenye staha"
Hakuna kitu kilicho bora kupita kingine (kuongea au Kunyamaza) Vyote vinaweza vikazalisha madhara katika jamii yetu, Cha muhimu ni kuzingatia katika mambo Matano niliyo bainisha hapo juu baada ya tafiti yangu Na tamani ukawe barozi kwa mwingine kumfikishia Tafiti.
Siku zote penda na adhimia kuwa "Taswira ambaeni fumbo kwao"
Mwandaaji :-
©tujuemoja
(David Daud Malunda)
MWANAFUNZI KATIKA CHUO CHA RUCU.

Upvote
1