Kukaa na funguo za choo cha boss nacho ni cheo

Kukaa na funguo za choo cha boss nacho ni cheo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna kijana kutoka kijijini alimaliza darasa la 12 na kufanikiwa kupata div IV. Alianza kilimo mpaka alipochoka kulima na kuamua kutafuta kibarua mjini. Kwa connection hapo alipofikia walimfahamu mzungu aliyetafuta msaidizi wa ndani. Yule kijana alipata kazi, na nyumba alipewa servants quarter, mshahara kima cha chini cha serikali na bima ya afya juu yake.

Baada ya mwaka mmoja alipata likizo. Alirudi kwao na zawadi nyingi. Wazazi wake walimpokea kwa furaha. Alikaa wiki mbili za likizo. Ndugu walikua bado na hamu nae. Walimuomba aongeze likizo, aliwaambia kuwa kazini anaaminika na kuhitajika sana maana hata funguo za chooni kwa boss anazishika yeye.
 

Kukaa na funguo za choo cha boss nacho ni cheo

..., aliwaambia kuwa kazini anaaminika na kuhitajika sana maana hata funguo za chooni kwa boss anazishika yeye.

Neno 'hata' linamaanisha kuwa kuna kazi nyingine anazozifanya, na hiyo ya kushika ufunguo wa choo cha boss ni mojawapo tu, na wala sio cheo kama ulivyoandika kwenye title (maana majukumu sio cheo, kwa sisi tunaofahamu utaratibu wa utendaji wa kazi). Kwa ufupi nilichogundua ni kwamba umeileta thread na kulazimisha wasomaji waelewe kile ulichodhamiria
 
Back
Top Bottom