Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
[h=2][/h]
Hatari ya Kukakamaa kwa mwili huongezeka kwa mtu mwenye kiharusi au vihatarishi vya kiharusi kutokana na utafiti uliofanywa Rotterdam uholanzi.
Sehemu ya ubongo kitaalamu Cerebral cortex inapokandamizwa aidha na kihararusi cha mishipa kuchanika na kuvujisha damu au mishipa inapoziba husababisha Kukakamaa kwa mwili. Hali yoyote isababishayo upungufu wa damu kufika katika sehemu za ubongo hupelekea Kukakamaa kwa mwili kutokea, na moja wapo ya sababu hizo ni magonjwa ya moyo.
Je ni magonjwa gani ya moyo husababisha Kukakamaa kwa mwili ?
Ni vitu gani vinaweza kuwa vihatarishi vya kupelekea Kukakamaa kwa mwili?
Vipimo gani vinashauriwa kufanywa japo mara mbili kwa mwaka?

- Shambulizi la moyo
- Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
- Shida ya misuli ya moyo
- Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo
- Upasuaji wa moyo
- Magonjwa ya valvu za moyo
- Moyo kupiga bila mpangilio
- Dawa za magonjwa ya moyo
Ni vitu gani vinaweza kuwa vihatarishi vya kupelekea Kukakamaa kwa mwili?
- Shinikizo la damu
- Kisukari
- Kuvuta sigara
- Cholesterol kuwa nyingi mwilini
- Historia ya familia kuwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kuziba
Vipimo gani vinashauriwa kufanywa japo mara mbili kwa mwaka?
- ECG
- Kipimo cha kujua wingi wa cholesterol mwilini
- Kipimo cha kisukari
- EEG chanzo.Kukakamaa kwa mwili kutokanako na magonjwa ya Moyo