Kukakamaa kwa mwili kutokanako na magonjwa ya moyo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[h=2][/h]


Hatari ya Kukakamaa kwa mwili huongezeka kwa mtu mwenye kiharusi au vihatarishi vya kiharusi kutokana na utafiti uliofanywa Rotterdam uholanzi.
Sehemu ya ubongo kitaalamu Cerebral cortex inapokandamizwa aidha na kihararusi cha mishipa kuchanika na kuvujisha damu au mishipa inapoziba husababisha Kukakamaa kwa mwili. Hali yoyote isababishayo upungufu wa damu kufika katika sehemu za ubongo hupelekea Kukakamaa kwa mwili kutokea, na moja wapo ya sababu hizo ni magonjwa ya moyo.


Je ni magonjwa gani ya moyo husababisha Kukakamaa kwa mwili ?

  • Shambulizi la moyo
  • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
  • Shida ya misuli ya moyo
  • Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo
  • Upasuaji wa moyo
  • Magonjwa ya valvu za moyo
  • Moyo kupiga bila mpangilio
  • Dawa za magonjwa ya moyo
Kwa watoto kunatatizo la mapigo ya moyo kupiga kupungua na saa nyingine kuongezeka kitaalamu Bradycardia tachycardia syndrome (sick sinus syndrome) hufananishwa na kifafa. Na kunatatizo jingine la moyo liitwalo kitaalamu Long QT syndrome ambalo husababisha Kukakamaa kwa mwili , kupoteza fahamu na hata kufa ghafla.
Ni vitu gani vinaweza kuwa vihatarishi vya kupelekea Kukakamaa kwa mwili?

  • Shinikizo la damu
  • Kisukari
  • Kuvuta sigara
  • Cholesterol kuwa nyingi mwilini
  • Historia ya familia kuwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kuziba

Vipimo gani vinashauriwa kufanywa japo mara mbili kwa mwaka?


 
Nashukuru kwa elimu hii,tatizo hili tiba yake ikoje hasa tiba mbadala...?
Kuna Maradhi mengine Dawa za Tiba Mbadala huwezi kuweka humu wazi na kuna Maradhi mengine unaweza kuweka humu ndani kwa manufaa ya watu wote bibie Mama timmy samahani uniwie radhi.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…