Elections 2010 Kukamatwa kwa kadi za ccm tunajifunza nini?

Elections 2010 Kukamatwa kwa kadi za ccm tunajifunza nini?

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
3,768
Reaction score
4,038
Ndugu wana JF salaamu. Mimi si mwanasiasa, ila naomba ushauri/majibu kwenu.
Kutokana na taharifa zinazotolewa na vyombo vya habari, pomoja na baadhi ya post ambozo zimewekwa humu JF, nimekuwa namaswali mengi ambayo nashindwa kupata majibu yake ipasavyo.
Baadhi ya maswali hayo ni kama haya:
1. Hivi kadi hizi ni feki au ni halali?
a) Kama ni feki, nategemea wahusika wangechukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kunyangwanywa sifa za kuwa kiongozi.

b) kama ni halali, je kwanini inaonekana si sahihi kugawa hizo kadi za chama chake kama amepata wanachama wapya ili kukipa nguvu chama chake?

2:Swali kubwa la pili: Katika habari hizi za kugawa kadi, sehemu kubwa kama si yote ni kadi za chama tawala CCM, je vyama vingine vimekumbwa na kasfa kama hiyo?

3:Nashindwa kupata jibu ikiwa wana chama wa chama kimoja wanafanyiana fitina na mizengwe hivyo, watafanyaje kwa cahama pinzani?

Mimi kwa mawazo yangu, naona kama CCM wanafanyiana hivyo wao kwa wao, basi ina maana ndiyo tabia yao ya wizi/kugushi katika mambo mengi na inaashiria hata katika kipindi cha kupiga kura uchaguzi mkuu, watafanya mambo hayo hayo ya kuiba karatasi za kura na ili washinde uchaguzi.

Naombeni mchango wenu.
 
Tunajifunza kuwa CCM ya sasa ni feki....wanachama feki......manifesto feki....viongozi feki....
 
mwenye macho haambiwi tazama.ndege wa rangi moja huruka pamoja.hiyo ndiyo ccm tuliyonayo sasa.baba wataifa angefufuka leo angehamia chadema.
 
Vijana wa vijiweni wananua sana kadi. wanazotumia kujiptia hela toka kwa wagombea. Wanajikusanya wanamfuata mgombea anamwaga posho ili apigiwe kura
 
Hivyi hizo kadi zinazo kamatwa zingekuwa za vyama vingine, serikali au vyombo vya seria vingefanya nini?
 
Inatueleza jinsi rangi yao ya ukweli ilivyo...
Madaraka yanayotafutwa kwa aina hii ni ngumu kuwa na ajenda ya maslahi kwa nchi...
Hawajali tena maisha ya mkulima na mfanyakazi bali ya chama,familia,jamaa...
Kuendelea kuongozwa na watu wenye mitizamo ya aina hii ni kujizidishia umaskini kwa miaka mingi ijayo..
 
Back
Top Bottom