Kukamatwa kwa Mbowe huenda kukabadili muelekeo kesi ya Sabaya

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Aliyekuwa DC wa Hai Ndg. Sabaya alifanikiwa mara kadhaa kudhibiti uhalifu na wahalifu wa Wilaya ya Hai waliotumia mgongo wa siasa.

Hata Mbowe mara kadhaa alidhibitiwa na wengi walisema mengi lakini kwa sasa ni dhahiri utagundua Mbowe alidekezwa na Sabaya, alidhibitiwa kwa heshima japo aliendelea kufadhili vijana kutengeneza maigizo.

Inasadikika mashahidi wengi kwenye kesi dhidi ya Sabaya ni wafuasi wa CHADEMA.

Kwa haya yanayoendelea sasa hivi dhidi ya Mbowe huenda yakabadili uelekeo dhidi ya kesi ya Sabaya. Huenda mashahidi wengi wakajiengua kwani muwezeshaji hayupo.
 
Gaidi Mbowe ametulizwa huko, nchi nzima imetulia, na viongozi wa serikali watapungua kufariki sasa kama Uamsho walivyo tulizwa na Zanzibar ikatulia.
 
Yaani kwa utoto mnaofanya vyombo vya dola vinajidhalilisha ile mbaya. Hivyo vyombo vimeshindwa kumkamata aliyejiunganishia bomba la mafuta, wako busy kufanya maigizo ya kitoto kuhusu Mbowe. Kwa mbahati mbaya wananchi wako digital, vyombo vya dola na serikali vimebaki analogia, ndio maana unafanyika utoto hadi wanafunzi wanashangaa. Acheni utoto maana katiba mpya ni lazima ipatikane.
 
Hakianani dunia inavituko kama mambo ya sabaya unayaona yalikuwa sahihi kwa sababu tu alidhibiti wapinzani na watu wenye mawazo ya kijinga kama yoko wakawa wengi katika nchi hii basi kazi ipo.
 
Gaidi Mbowe ametulizwa huko, nchi nzima imetulia, na viongozi wa serikali watapungua kufariki sasa kama Uamsho walivyo tulizwa na Zanzibar ikatulia.

Mwanzoni nilikuwa nakereka kweli nikisikia wazungu wanatuita manyani, ila kwa huu upuuzi unaofanywa na vyombo vya dola naona wako sahihi mno.
 
Na tozo kama kawaida sasa ...Mwigulu atapata usingizi
 
Mwanzoni nilikuwa nakereka kweli nikisikia wazungu wanatuita manyani, ila kwa huu upuuzi unaofanywa na vyombo vya dola naona wako sahihi mno.
Tunampelekea uji saa ngapi Gaidi Mbowe, Tanzania itatulia sasa kama Zanzibar ilivyotulia baada ya magaidi wa uamsho kuwekwa sehemu salama.
 
Mwanzoni nilikuwa nakereka kweli nikisikia wazungu wanatuita manyani, ila kwa huu upuuzi unaofanywa na vyombo vya dola naona wako sahihi mno.
Kabisa, yaani CCM na serikali yake haijagundua kuwa wanathibitisha kuwa wao ni manyani mbele ya use wa dunia?
Screenshot_20210723-103638_Twitter.jpg
 
Kumbe ndiyo maana yake! Akamatwe mbowe ili mashahidi wa kesi ya sabaya wakose nguvu. Dunia Ina vituko
 
Kamanda jenga hoja
Yaani kwa utoto mnaofanya vyombo vya dola vinajidhalilisha ile mbaya. Hivyo vyombo vimeshindwa kumkamata aliyejiunganishia bomba la mafuta, wako busy kufanya maigizo ya kitoto kuhusu Mbowe. Kwa mbahati mbaya wananchi wako digital, vyombo vya dola na serikali vimebaki analogia, ndio maana unafanyika utoto hadi wanafunzi wanashangaa. Acheni utoto maana katiba mpya ni lazima ipatikane.
 
Ndugu zangu,

Aliyekuwa DC wa Hai Ndg. Sabaya alifanikiwa mara kadhaa kudhibiti uhalifu na wahalifu wa Wilaya ya Hai waliotumia mgongo wa siasa.

Hata Mbowe mara kadhaa alidhibitiwa na wengi walisema mengi lakini kwa sasa ni dhahiri utagundua Mbowe alidekezwa na Sabaya, alidhibitiwa kwa heshima japo aliendelea kufadhili vijana kutengeneza maigizo.

Inasadikika mashahidi wengi kwenye kesi dhidi ya Sabaya ni wafuasi wa Chadema.

Kwa haya yanayoendelea sasa hivi dhidi ya Mbowe huenda yakabadili uelekeo dhidi ya kesi ya Sabaya. Huenda mashahidi wengi wakajiengua kwani muwezeshaji hayupo.
Sasa ndiyo umeandika nini hapa? Yaani Mbowe Mbowe tu
 
Back
Top Bottom