Kukamatwa kwa mzungu muuzaji wa solar panel kwa wavuvi,imekaaje hii?

Kukamatwa kwa mzungu muuzaji wa solar panel kwa wavuvi,imekaaje hii?

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,229
Kuna video ina trend, twitter inamuonesha ofisa mmoja wa serikali akiwa na waandishi wa habari kwenye ofisi ya kampuni inayomilikiwa na mama wa kizungu mmoja wakijibizana kwa madai kuwa kampuni hiyo ina kosa la kuwauzia wavuvi vifaa vya sola bila kupata kibali cha wizara ya uvuvi.

Watu wanajiuliza ina maana mteja akija kununua kitu kwangu inabid nimuulize kama yeye ni mvuvi au lah? ili kama ni mvuvi niende wizarani niombe kibali kwanza au?

Wanajiuliza zaid tena ina maana katika dunia hii ya sasa ambayo kuna mkazo mkubwa sana unaendelea juu ya matumizi vyanzo mbadala vya nishati, na kama ada, nishati ya jua inapewa mkazo sana, serikali yetu ina weka kauzibe katika kuuza vifaa hivyo??

Wengine wanauliza, hivi hawa maofisa wetu hawawezi kwenda mahali bila media, sababu now we have this video trending, ikimuonesha the so called mwekezaji akijibishana na ofisa wetu, kwa kitu ambacho kwa kwa judgement ya haraka inaonekana kama mwekezaji anafanya kazi kwenye mazingira magumu yanayotengenezwa na mifumo yetu.

Anyway watu wanaongea mengi ila mimi, naomba kwa waelewa wa hii sheria wanielekeze kosa katika muktadha huo ni lipi?
 
Yaan tanzania siku izi sijui imekuwaje!? Yaani ni unoko karibu kila sekta!hyo taa utadhani wavuvi wanaenda kuzitumia kuulia samaki
 
Watafute njia nyingie bhnaa yani huo ni ubata,kwan mtu ayashindwaje kunnua akisema yeye anajitaji ya matumiz yake kwake afu na akatumia kwenye uvuvi that is nonesense
 
Inasikitisha, hao wawekezaji wanakuja kutafuta fursa
 
Niliona hiyo habar star TV nikajiuliza maswali kwa mfano Nikifungua Duka LA kuuza zile shemli au Duka LA taa za solar nikaombe kibali wizara ya uvivu ?? Inawahusu nini Kwani taa ni za kumulikia ngombe tu? Au samaki tu? Mbona tukienda kwa koti hakimu atawashangaa
 
Huyu afisa kiki au afisa samaki? mimi dukani kwangu nauza vitu vya nyumbani ikiwemo na kisu. Sasa mteja akinunua kisu kwangu akaenda kuchoma nayo mtu huko kwenye ogomvi wao itabidi nikamatwe maana jamaa katumia kisu kuchoma mtu na sio kumenyea maembe?
 
Tumekuwa Taifa la mataahira! Sasa hivi viongozi wengi wanaiga kichaa cha kiongozi wao! Ina maana siku hizi wavuvi hawatuhusiwi kumiliki taa za solar? Mbona huku mtaani wakulima wanauziwa solar bila kibali cha wizara ya kilimo? Huu ni ukumanina!
 
Huyu Mama aachiwe mara moja
Sijui sheria inasemaje ila akili ya haraharaka ni kwamba biashara ya solar panel si ni kma biashara nyengine tu za hardware na nyenginezo.

Nahisi muhimu si ni kua na kibali cha biashara na kma kibali anacho bas hapo hakuna la kumkamatia pia dukani kwangu akija mteja hta kma ni mvuvi nisimuuzie?

Haya maisha tunarejeshna nyumba kwasababu zisizo za msingi. Wanataka tue na utamaduni ule ule wakutumia makarabia na nyenzo hafifu wakati mambo yamerahisishwa.

Au kma wavuvi kuvua lbda kisichofaa hilo ni kosa lao wenyew wavuvi lkini biashara kma ilivyo ya kuwauzia solar panel hmna tatizo.
 
Kuna video ina trend, twitter inamuonesha ofisa mmoja wa serikali akiwa na waandishi wa habari kwenye ofisi ya kampuni inayomilikiwa na mama wa kizungu mmoja wakijibizana kwa madai kuwa kampuni hiyo ina kosa la kuwauzia wavuvi vifaa vya sola bila kupata kibali cha wizara ya uvuvi.

Watu wanajiuliza ina maana mteja akija kununua kitu kwangu inabid nimuulize kama yeye ni mvuvi au lah? ili kama ni mvuvi niende wizarani niombe kibali kwanza au?

Wanajiuliza zaid tena ina maana katika dunia hii ya sasa ambayo kuna mkazo mkubwa sana unaendelea juu ya matumizi vyanzo mbadala vya nishati, na kama ada, nishati ya jua inapewa mkazo sana, serikali yetu ina weka kauzibe katika kuuza vifaa hivyo??

Wengine wanauliza, hivi hawa maofisa wetu hawawezi kwenda mahali bila media, sababu now we have this video trending, ikimuonesha the so called mwekezaji akijibishana na ofisa wetu, kwa kitu ambacho kwa kwa judgement ya haraka inaonekana kama mwekezaji anafanya kazi kwenye mazingira magumu yanayotengenezwa na mifumo yetu.

Anyway watu wanaongea mengi ila mimi, naomba kwa waelewa wa hii sheria wanielekeze kosa katika muktadha huo ni lipi?

Du! Ina maana hata wanaowauzia wavuvi subwoofer wanahitaji kibali cha Wizara ya Uvuvi?
 
muuza duka si mwekezaji mkuu, hiyo kazi inaweza fanya na mzawa
 
Solar ni non renewable energy zamani wavuvi walikua wanatumia karabai zinakula mafuta ya taa balaa gharama ni kubwa pia kuchafua mazingira sasa solar ndiyo solution na ni rahisi kwa mvuvi.Tochi za betri ni gharama balaa.
Mtu anakuja anakuambia aganye research kwanza jee wavuvi wakavue giza????au warudie karabai?
Kuwekeza tanzania ni mgumu sana taasisi za umma hazimsaidii mwananchi bali zinawaza mapato tuu ambayo siyo sustainable
 
Enzi hzo karabai linatumia Lita 1 ya mafuta ya taa kwa usiku mzima,na Sikh zingne tulikuwa tunapata dagaa waliomwagikiwa mafuta ya taa,sasa solar imepunguza gharama afu kuna mjinga na mihemko yake ya kutaka kuonekana anafanya kazi anakuja kuzingua,ni bora kuwa na viongozi wasiokuwa na elimu kubwa,mpaka sasa sijaona faida ya elimu zao kubwa ktk taifa hili.
 
Back
Top Bottom