Kukamatwa silaha za Emirati Uganda kwaashiria nini Uwekezaji wa DP World nchini?

Kukamatwa silaha za Emirati Uganda kwaashiria nini Uwekezaji wa DP World nchini?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Tarehe 02nd June 2023, maofisa wa uhamiaji wa Uganda walikamata silaha za Falme za Kiarabu (UAE) zikipelekwa Sudani kupitia Chad kulingana na makala ya WSJ (Wall Street Journal) ya leo tarehe 10th August 2023.

Maafisa walionasa hizo silaha hizo walipowajuza mabosi zao hatua zipi wachukue walijibiwa wawaruhusu na wasipige picha silaha hizo na kuanzia hapo ndege za UAE zitakuwa zikishughulikiwa na wizara ya ulinzi. Safari za ndege za Falme za Kiarabu kwenda Sudan kupitia Chad zimeongezeka maradufu.

Kulingana na makala ya WSJ, Falme za Kiarabu zinamsaidia jenerali muasi anayeitwa Mohamed Hamdan Dagalo ambaye anapigana vita kumwondoa mtawala wa kijeshi wa nchi hiyo anayeitwa

Gazeti la Marekani la WSJ linasema Falme za Kiarabu zinampa jenerali Dagalo misaada ya kijeshi ili kulinda uwekezaji wao wa bandari, uchimbaji wa dhahabu, umiliki wa mashamba n.k wa kadhalika.

The U.A.E. is likely betting on Dagalo to help protect Emirati interests in Sudan, with its strategic location on the Red Sea, access to the Nile River and vast gold reserves. The U.A.E.’s interests include swaths of Sudanese farmland and a stake in a planned $6 billion port on the Red Sea…….


…..In one of the latest deliveries, trucks loaded with military suppliesfrom the U.A.E. left Amdjarass airport the final week of July for Sudan’s Al-Zarq area, an RSF stronghold in northern Darfur, the African official and a former U.S. official said.

Sisi tunaona uwekezaji wa DP WORLD ni hatarishi kwa uhuru wetu (sovereignty).

Sasa chaguzi zetu zitakuwa zinaingiliwa na pesa za Falme za Kiarabu ili kulinda uwekezaji wao.

Tutashangaa kama mwaka huu utaisha kama NAFCO na NDC hazitafutwa na mashamba yao na ardhi yao yote hawatauziwa waarabu wa Falme za Kiarabu maana wana nia ya kumiliki ardhi kwa ajili ya kilimo na kuwalisha raia wao. Pia tutashangaa kama hawatamilikishwa migodi mingi kwa kulindwa na sheria wasilipe kodi.
 
Nilipoona tu hii Habari nikawakumbuka na Somali Pirates walipoteka meli kumbe imejaa silaha zikiwa zimeandikwa mzigo wa Kenya kumbe ilikuwa ni diverted tu na documents ni mzigo wa South Sudan kwa kina Garang
Dunia hii ina mambo mengi sana, na wote ni kwa ajili ya matumbo yao na ni biashara haramu
 
Hao waarabu ni mashetani kamili, wanaonesha dhamira yao ovu kuzitawala hizi nchi kwa njia yoyote, huku wajinga wanawashangilia.
Watu wapo sudan, chad na uganda
Nyie huku mnatetemeka? 😂😂👍👍👍🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kweli mzungu amewaharibu
 
Watu wapo sudan, chad na uganda
Nyie huku mnatetemeka? [emoji23][emoji23][emoji106][emoji106][emoji106][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kweli mzungu amewaharibu
Wanapeleka silaha Sudani ili kulinda uwekezaji wao wa bandari sasa hapa kwetu huoni tumenunua machafuko?
 
Mengi yanakuja Mana ukichukua tatizo linaharika na wenzie.
 
Hao waarabu ni mashetani kamili, wanaonesha dhamira yao ovu kuzitawala hizi nchi kwa njia yoyote, huku wajinga wanawashangilia.
Hapa mpaka damu ianze kumwagika ndipo tutaelewa maana ya umuhimu kwa uhuru wetu sisi wenyewe tukasimamia njia kuu za uchumi.
 
U.A.E ni moja ya nchi mbaya sana hata ukanda wake wenyewe wa Uarabuni. Kwanza ina arms industry inayokua na hasa ilifanya kuiba wanasayansi kwingineko duniani kama South Africa. Ikishindwa kutengeneza silaha haioni shida kununua kwingineko ikazituma kwenye eneo la vita, wananunua silaha China, Russia, Turkey wanazituma kwenye machafuko.
Pale Libya wametuma hadi Pantsir air defence systems za Urusi. Sudan hapo wamejaza silaha zao na za kigeni walizonunua na hazipiti Uganda peke yake hata Chad zinapita ambapo U.A.E wana influence.
Hao Uganda wanazo silaha kadhaa wamenunua Dubai.

Hii ni Turkish made grenade launcher imeuzwa U.A.E inatumika na RFS wa Sudan, na haikuwa kwenye inventory ya Sudanese forces kusema waasi wameiiba
20230810_134109.jpg
 
Back
Top Bottom