Kukamilika kwa Mradi wa Umeme Rusumo Kunazidi Kuimarisha Gridi ya Taifa - Kamati ya Bunge

Kukamilika kwa Mradi wa Umeme Rusumo Kunazidi Kuimarisha Gridi ya Taifa - Kamati ya Bunge

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.51.jpeg

📌 Ni mradi wa megawati 80 unaotekelezwa na Tanzania, Burundi, Rwanda

📌 Kila nchi yafaidika na megawati 26.6

📌 Kamati yasema mradi utazidi kuimarisha uhusiano mzuri wa Tanzania, Burundi, Rwanda

Imeelezwa kuwa, mradi wa kufua umeme unaotokana na maji wa Rusumo, umeanza kuzalisha megawati 80 ambazo zinagawanywa kwa usawa wa megawati 26.6 kwa nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi na hivyo kuzidi kuimarisha gridi za Taifa za umeme.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Kilumbe Ng'enda, amesema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo uliopo Wilaya ya Ngara katika Mkoa wa Kagera.

WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.54.jpeg

Amesema mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya RPCL inayomilikiwa na nchi zote tatu ni kielelezo cha azma ya Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kijamii.

Aidha, Mhe. Ng'enda amewataka watekelezaji wa mradi kuendelea kufanya kazi kwa tija na kuhakikisha matumizi ya fedha yanaendana na maendeleo ya mradi, pia umuhimu wa kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi ya kijamii (CSR).

WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.55.jpeg

Kamati imeeleza kuridhishwa kwake na mafanikio ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika uendeshaji wa pamoja, jambo litakalosaidia kuimarisha pia uhusiano mzuri baina ya nchi hizo tatu.

Vilevile Kamati imepongeza ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania, Burundi na Rwanda katika kuchochea maendeleo ya uchumi na kudumisha amani, undugu na urafiki wa nchi hizo.

WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.56.jpeg

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt.Khatibu Kazungu, amewashukuru Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kwa ufuatiliaji na ukaguzi wa mradi huo ambao una maslahi mapana kwa Taifa zima.

Aidha, ameahidi kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuyafanyia kazi maelekezo yanayotolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo ili kuzidi kuongeza ufanisi wa Sekta ya Nishati.

WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.57.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.58.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-11-12 at 18.49.03.mp4
    28.8 MB
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.51 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.51 (1).jpeg
    207 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.52.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.52.jpeg
    470.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.53.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.53.jpeg
    264.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.58 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.58 (1).jpeg
    640.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.48.59.jpeg
    364.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.00.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.00.jpeg
    448.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.01.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.01.jpeg
    460.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-12 at 18.49.02.jpeg
    301.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom