Kukata tamaa ni dhambi

Utajua wewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2024
Posts
928
Reaction score
1,836
Kama wewe ni jobless na maisha yamekuchapa,usivunjike moyo wala usikate tamaa
Ipo siku moja na wewe utakufa.
Ni lazima tuweze kuelewa nyakati na mabadiliko ya kidunia.

Tunaishi katika kizazi ambacho
a)Elimu sio kigezo cha kuajiriwa
b)Biashara zinauliwa na ushuru
c)Mishahara hailingani na gharama ya maisha

Alafu wazee tunawakejeli sana kwamba vijana wazembe tumesahau enzi zetu
a)Form 4 waliajiriwa wizarani
b)Viwanja viliuzwa bei 5k
c)ushuru hauku uwa biashara

Kwanza poleni kwa kukosa Maarifa
Umeishi maisha yako yote ukiamini kuna kanuni kwenye maisha.Nature haiitaji sheria za kibinadamu.

Elimu ya vyeti mnayoisoma ni nzuri ,ila ujuzi ni muhimu zaidi .
Ili siku ukikosa ajira kutokana na vyeti vyenu unapata kazi kutokana na ujuzi wako.(Elimu sio lazima uipate darasani usikariri na ujue kua degree sio kigezo cha maisha mazuri )
Ila ni uwezo wa kubadilisha elimu yako kuwa pesa ( ndio maana siku hizi wadada wenye matako makubwa wanajiamini kuliko mwenye degree)

Kingine usikae ndani tu ,toka jichanganye na wenzio maana RIZIKI YA MBWA IPO MIGUUNI PAKE( Na mkaa bure sio sawa na mtembea bure)

Hakikisha unajitahidi kuishi na watu vizuri kuna muda heshima na nidhamu inaweza kukupeleka sehemu ambayo bidii haiwezi kukufikisha.

Kauli ya "watanionaje "itakuuwa na njaa.
Kwa niaba ya wanaokutegemea usikate Tamaa.
Eka mbali vitu vinavyokurudisha nyuma kama uzizi na ulevi.

Nakumbuka ukianza safari ya kuboresha maisha yako ,basi"kutoeleweka na watu" ndio gharama ambayo itakubidi ulipie.

Jua unataka nini ? Anza kukipambania ,sisi wenyewe tumetoka kwa kilimo .
Muombe Mungu akure moyo wa uvumilivu,tuvumilie yote tunayopitia.
Na akuepushe na husda za wanadamu akufungulie milango ya ridhiki
Na akujalie mwisho mwema.

Elimu ni ufunguo wa maisha ni kweli ila inategemea ni elimu kuhusu nini? Tatizo elimu zetu zinafundisha watu kuwa wa pambanaji zaidi ya watafutaji.
Elimu sio lazima uipate darasani siku hizi kuna mitandao kibao youtube ,n.k

"Hard Times create strong man"I know the system is hard for the poor,usikate tamaa pamba uwezavyo kijana .

Najua utajiri na umaskini haupo kwenye mazingira tu bali upo akilini( try to have positive mentality) .

Mafanikio na furaha haviangaikiwi vinakuja kama matokeo.

Rich is Principlal, rules and displaces
Wealth is spiritual.

Na kamwe usiruhusu sauti za njee ziamue hatima yako .
Kila unachokitaka kipo lakini kimefichwa ndani ya muda kuwa mvumilivu.


"Ipo siku moja mtakuja shangaa ng'ombe wa maskini kazaa"


Ubaya ubwela
 
Siyo dhambi, bali ni dhambi kubwa sana.

Kukata tamaa ni nusu ya kujiombea kifo.
 
Kukata Tamaa marufuku,hakuna formula ya kujinasua na Umaskini,pambana ungali hai, msingi wa wa yote ni Afya NJEMA,maradhi Safi.Uhuru ulipatikana kwa kupambana na ulipatikana kwa nchi Nyingi Duniani.Kwa maisha ni hivyo hivyo kupambana pasipo kukata Tamaa.
 
Mkuu umetisha sana👊
Ubaya ubwela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…