Kukataliwa na kutupwa kwa parachichi za Tanzania kule Afrika Kusini nini tunajifunza?

Kukataliwa na kutupwa kwa parachichi za Tanzania kule Afrika Kusini nini tunajifunza?

Status
Not open for further replies.

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Waziri wa kilimo ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii.

Kuwa maparachichi yaliyo enda kuuzwa nchini Afrika ya kusini kutokea Tanzania yamekataliwa na kutupwa kutokana na mapungufu ya ubora unao hitajika ikiwemo kuchumwa yakiwa bado machanga au hayaja komaa vizuri.

Je lawama apewe nani kati ya mkulima na mnunuzi au maafisa wa ugani?

Tunajifunza nini kwa hili?
Screenshot_20220122-203910.jpg


=====

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekanusha Habari hii

======
Hii SI habari ya kweli, ni picha za mwaka 2020

Oda za kwenda Afrika kusini zipo, zinaendelea vizuri na zinaongezeka, na tuna habari njema ya kuanza maongezi na nchi ya India.

Hizi habari za UONGO, na zipuuzwe.
Screenshot_20220122-211816.png
 
Duh poleni wajasiliamali wenzetu, hakuna kurudi nyuma. Wataalamu wasaidie kushauri namna Bora ya kuwa na bidhaa zenye viwango wakati wa kuuza nje.
 
Wajitathimini...naamini safari nyingine hawata rudia huu upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Africa kusini ,sio Kenya ,au Uganda ,au Burundi ,kule kila kitu n8 standard,Sasa hawa wafanyab8ashara wankwetu,walijua wanapeleka uganda,!! jifunzeni kutimiza standard za kimataifa .
 
Tabia za kitanzania za kutotimiza wajibu na kutowakibika ipasavyo ni hasara kwa taifa na Dunia nzima.
Hili jambo nadhani linapaswa kuwa fundisho tosha kwa wahusika ili wakati mwingine wasifanye haya makosa.
 
Wajitathimini...naamini safari nyingine hawata rudia huu upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu huoni kama hili linaweza kuwafanya hao wanunuzi wa products zetu wakawa na mashaka na hizo bidhaa kutoka Tanzania?
 
Hili jambo nadhani linapaswa kuwa fundisho tosha kwa wahusika ili wakati mwingine wasifanye haya makosa.
Hapo ukiangalia gharama ya kuajiri wataalamu wakilimo Ili kuepuka hasara za hivi , na gharama za kuwatumia madalali makanjanja Kwa maana ya 10% kwa weledi wetu tunaweza Sema kutumia wataalamu ni hasara na nibora kuendelea na makanjanja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom