Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

LowassA aende upinzaniiiiiii

Akafanye nini yeye na GENGE lake sindio mabingwa wakuponda wapinza sasa kwakuwa kamwagika huku afanye kimbilio lake?? Hapana wacha akachunge mbuzi MONDULI
 
Pasco....pole kaka
Hata ingekuwa mie ningepanic...
 
Last edited by a moderator:
Hameni huko enyi mlio CCM. Tokeni kwake anyi mataifa, msishiriki dhambi ya CCM!
 
Pasco

Wala hujakosea, Lowasa ni kipenzi cha wengi na waliomkata wanampenda zaidi ndiyo maana wakamkata, wamemuonea huruma, Lowasa ni mgonjwa na wangembebesha mzigo mkubwa sana zaidi ya uwezo wake.

Kwa hiyo usisikitike, kama kweli unampenda Lowasa basi ulitakiwa ufurahi.

Mimi nimefurahi.
 
haraka sana lowassa wewe ni jiwe kuu,njoo ukawa na team yako.Tushinde vita hii.

Mkuu UKAWA sio shimo la takataka hao sinimabingwa wakukashifu Upinzani Leo aje kufanya nini anzishenj chama Chenu ikishindikana aende Monduli akaongoze Mifugo
 

Atafanya la maana sana kama ile hadithi ya Richmond ambayo kila siku anasema ndio iliyomchafua akaja na ukweli wake hadharani tumjue muhusika halisi. Maana alisema alikubali kubeba msalaba ili kuiokoa serikali. Na mtu mzima kama yeye na aliyekuwa na madaraka ya PM akisema kuiokoa serikali, wenye akili wanajua kuwa alimaanisha kumuokoa nani.
Sasa kwa vile wamemuaibisha hata jina halikupelekwa KK naye sasa aaibishe.
 

Sema kabisa aende ACT, maana alishakaribishwa huko. Yeye na Mwigulu muda si mrefu tutawasikia wakitia timu. Ndipo litakapotimia lile lililopatwa kunenwa kwa kinywa cha binadamu kuwa ACT iliundwa kimkakati...

Kuhusiana na kujiandaa, yeye alikuwa anafanya maandalizi ya namna gani? kama CCM yenyewe imesema usifanye hiki, wewe ukaamua kukaidi, utakatwa tu! Na kama anataka kufanya siasa za Marekani kama unavyosema, angechukua kadi ya Republican au Democrat...

CCM ina wenyewe bwana..na yeye ni mmoja wao tena kwa miaka mingi, nashangaa hakulijua hilo. Labda amezeeka kwa hiyo mambo mengine ya msingi anayasahau.
 

Mmoja wa wenyeviti wenza wa UKAWA Dk Slaa 2007 pale mwembe Yanga alitoa orodha ya list of shame na katika main a ya mafisadi papa Lowassa alikuwa mmojawapo,kipi kinakufanya one kuwa hapo wapinzani wanaweza wakala matapishi yao?

Au unamaanisha upinzani tu wowote? naona tulimsikia ZZK akimwambia Wako tayari kumuachia kugombea urais iwapo atatangaza Mali zake. Nadhani ifike wakati watanzania tukaamka kutoka kwenye huu upofu na tujue chanzo cha tatizo la mkwamo wetu halafu tuchanganue kweli Lowassa ndani ya CCM akiiwa rais anaweza akatuletea maendeleo kama au ikiwezekana kuwapita hata Kenya
 

Ugonjwa wa mtu anaujua yeye mwenyewe na daktari wake. Yeye kesha sema kuwa yuko fit, na hakuna daktari aliyejitokeza kutamka kuwa Lowasa ni mgonjwa wewe na wenzako hiyo huruma yenu imetokea wapi?
Hapo ni mdumange tuu lazima muucheze.
 
Washabiki wa ufisadi ni wachache sana ila sauti zao zina nguvu sana kama radi bali wanaochukia ufisadi ni wengi sana bali hawana sauti na nguvu yao iko kwenye kura.
 
Mkuu hata kwenye list of shame hukusikia jina lake au ushabiki unakutia upofu.
 
Lowassa hajakatwa na CC kakatwa na kamati ya maadili ambayo haipo kikatiba

Kukatwa ni kukatwa tu, limetumika "PANGA" au "SHOKA" hivyo ni vitendea kazi tu vilivyotumika na "MKATAJI", wa kunielewa watanielewa.
 
Pasco

Unaandika sana na kimsingi unaweka wazi unachokiamini; ila naona unajitambulisha zaidi na personality unazozijenga kwa uandishi wako zaidi ya facts on the ground. Mwamba wako umebomolewa kama mnara wa Babeli lugha gongana.

Ni wakati muafaka sasa atuambie hadharani alipo Daudi Balali
 
Yani wewe Pasco uzee unakuingia vibaya sana unatabia za kinafiki nafiki!
 
Last edited by a moderator:
Inanikumbusha wale ambao walikua wanajenga mnala wa babeli wamfuate mungu alifikiria akaona hawa watu hawana akili wananifuata mbinguni wakati nipo nao duniani akamua kuwatenganisha

Kwanza akawapumbaza akili fundi akiagiza jiwe mtu analeta mchanga ukiagiza maji analeta tofali hii yote ilikua kuwatenganisha .

Na hichi ndicho kilocho wapata ccm na historia imejiludia mara mbili ila wao hili swala hawalijui kwasababu. Huu ni mpango wa Mungu.

Na kwa kuitia hili ukawa ushindi ule pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…