Kukatwa Misaada toka USAID kilio ni kikubwa!

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
1. Kukatwa kwa Msaada wa takribani Trillioni 1 TZS kwenye sekta ya Afya/Elimu kwa mwaka. Hilo litaumiza kila mtu, tusifurahie kindezi.

2. Sekta nyingine kama TRA (income tax), Health insurance, general insurance, mabenki (mikopo ya wafanyakazi), domestic airlines, kampuni za Magari zote zinakwenda kulia)).
 
Kwani msaada huu umekatwa Tanzania pekee au dunia nzima maana kwa mara ya kwanza naona watu wanalia kwa kukosa hisani kama nchi ndio ibane matumizi na kujitahidi kusaidia raia wake kwa namna yeyote mawaziri wanatapanya pes kwa kununua magari ya gharama na matimu ya mipira mahekalu ufukweni!
 
Reactions: apk
Hapa ndiyo tunajua kama tuna viongozi wasomi au vilaza acheni tuanze kuitegemea...hizo degree zao za uchumi hapa ndipo sehemu muhimu pa kufanyia kazi, mtegemea cha ndugu hufa masikini waswahili walisema
Trump anafanya vyema, hii itasaidia sana kuwafanya waAfrika wengi(hususani Watu weusi) kuanza kuwa na akili nzuri ya kuweza kujitegemea wao wenyewe.
Hata Watawala waliopo watakuwa na Heshima na nidhamu ya hali ya juu kabisa katika Matumizi ya Fedha za Kodi za Wananchi.
Siyo siri hata kidogo,Watawala karibia wote kabisa wa nchi za Afrika hawana kabisa nidhamu nzuri ya hali ya juu katika Matumizi ya Fedha za Kodi za Wananchi waliopo katika nchi zao. Watawala wengi sana ni Wezi, Mafisadi, Wafujaji Sana wa Fedha za Kodi, n.k.
Tazama msafara huu wa Kiongozi huyu wa nchi fulani hapa Afrika kisha jiulize:- Je, ni gharama kubwa kiasi gani ilitumika kwenye msafara huu wa anasa? Je, kuna ULAZIMA wowote ule wa kuwa na misafafara kama hii kwenye nchi hiyo ambayo Bajeti yake ya kila Mwaka hutegemea Misaada kutoka Marekani na washirika wake? Je, Wananchi wa kawaida waliopo katika nchi hiyo wanaweza kupata faida gani hasa kutokana na misafafara yenye misururu mirefu ya magari kama huu?

Tafakari, Chukua Hatua!
 

Attachments

  • 5771391-6b7300c48c43013b94b420cc6e416c60.mp4
    8.3 MB
Matumizi mabaya Sana ya Fedha za Kodi za Wananchi, Matumizi ya anasa na ya kufuru yasiyofaa, yasiyokuwa na tija yoyote ile kwa Wananchi walipakodi.
 

Attachments

  • 5771391-6b7300c48c43013b94b420cc6e416c60.mp4
    8.3 MB
Misaada inakwenda kukatwa, huenda na nchi za ulaya nazo zikafuata mkumbo huo, nasi sasa tupunguze mishahara minono ile mishahara ya 10m+,yote isiwepo serekalini
 
Kama ngedere kushangilia kifo cha mwenye shamba la mahindi, tuna shida sana wabongo!
 
Trump njoo umulike na huku kuna mafisadi kibao wameiba fedha za umma na hizo ulizokuwa unatoa misaada wakajenga vituo vingi vya mafuta na nyingine wameficha akaunti za nje ili kuwaandalia mazingira watoto wao kugombea urais au kuwa viongozi huko mbeleni.
 
Hapa ndiyo tunajua kama tuna viongozi wasomi au vilaza acheni tuanze kuitegemea...hizo degree zao za uchumi hapa ndipo sehemu muhimu pa kufanyia kazi, mtegemea cha ndugu hufa masikini waswahili walisema
Kama kawaida natarajia haya yafuatayo:

Kupanda kwa bei za bundle,
Kuongezeka bei ya luku na hela ya mwezi wa jengo ,
Kupanda kwa bei ya mafuta na nauli ,
Hawachomoki humo mkuu.

Lakini kusema mwaka huu hatununui v8 hawawazii hilo kuna mbunge mmoja alisema kila laini ikatwe Tsh 500 ili kila mtanzania apate bima ya afya ila nchi yangu.

TANZANIA HATUJAWAHI KUWA NA TATIZO LA HELA TUNA TATIZO LA USIMAMIZI MBOVU NA WIZI WA FEDHA ZA UMMA BASI.

Watu kila siku wanatajwa na CAG wanakula hela lakini ndio kwanza wengine wapo mpaka leo tena viongozi wanadunda yaani hela inayoliwa ni nyingi kuliko inayoenda kwenye miradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…