A
Anonymous
Guest
Fikiria unatafuta ajira ili upate pesa, mwingine anakwambia utoe pesa ili upate ajira.
Kwa wale wenzangu na mimi mtakuwa mnaelewa machungu ya kuambiwa hivyo ili hali mfukoni huna hata mia na hujui utapata wapi nauli ya kurudia geto wala msosi wa usiku.
Ndani ya mradi wa ujenzi wa barabara ya mwendokasi awamu ya nne loti 2 kutoka mwenge mpaka tegeta (dawasa) unao fadhiliwa na benki ya dunia kumekuwa na rushwa iliyokithiri.
Katika mradi huo kampuni ya ujenzi ya SHANDOG LUQUIAO GROUP CO.LTD kutoka china ndio mtekelezaji mkuu wa mradi huo, kempu yao ipo karibu na mataa ya kawe opposite na fremu za jeshi hapa Lugalo karibu na kituo cha daladala cha bondeni.

Kumekuwa na vitendo vya rushwa ambavyo havivumiliki kutoka kwa HR wakibongo wa kampuni hiyo akiwataka waombaji wa nafasi za kazi kutoa rushwa ili wapate ajira bila hivyo utachelewa sana kupata kazi au usipate kabisa.
Ikiwa wewe ni kibarua au saidia fundi unatakiwa kutoa laki moja mafundi au dereva au operator wanatakiwa kutoa laki moja na hamsini mpaka laki mbili na hana huruma na sura ya mtu.
Hali hiyo ya kukithiri kwa rushwa imepelekea watu kutoka mikoa ya mbali kuajiriwa kwa wingi huku wakazi wengi wa maeneo hayo kukosa nafasi ili hali sera, sheria na kanuni za nchi zinataka wao kupewa kipaumbele zaidi.
Mbaya zaidi HR huyu anajenga chuki kubwa sana kati ya wale wanaotoa rushwa na wale waliokataa kutoa wakiamini kupata kazi bila hongo ni haki yao kama Watanzania.
Unaeza kuta mtu mmesota naye miezi mitatu au mitano mkiwa marafiki mkisubiri nafasi ya kazi.
Ila kwa bahati mbaya yeye akafanikiwa kuingia kabla yako kwa kutumia rushwa, aisee akitoka hapo sio rafiki yako tena na akikuona anakukimbia kama hakujui.
Ukimuuliza kwanini unafanya hiyo anakwambia ndio tulivyoambiwa na HR tusiongee na ninyi.
Hali kama hiyo ya rushwa iliwahi kutokea miezi minne iliyopita kwenye moja ya kempu iliyopo karibu na bar ya 360 ukitokea mwenge kuelekea tegeta hapa maeneo ya Lugalo.
Ambapo vibarua, madereva na mafundi walitaka kutolewa kazini kiujanja ujanja ili waingize watu wao waliotoa rushwa kwa HR.
Watu wakagoma, baadae baadhi ya wanajeshi kutoka Lugalo wakaingilia sakata hilo na kulizima kimya kimya kwa vitisho visivyokuwa na tija kwa vibarua, madereva na mafundi ambao ilikuwa haki yao kuwa kazini kwa wakati huo.
Tunaomba wahusika waingilie kati swala hili, ili kila mwananchi apate haki yake kabla hali haijawa mbaya zaidi.
~SAIDIENI JAMII