KERO Kukithiri kwa michango ya ovyo shule ya sekondari Itega jijini Dodoma

KERO Kukithiri kwa michango ya ovyo shule ya sekondari Itega jijini Dodoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na adhabu kali na kauli mbaya zinazotolewa na baadhi ya Walimu kwa watoto wetu pale ambapo mzazi hajatoa kiasi cha Tsh 2,000 kila wiki kwaajili ya masomo ya remidial na hatushirikishwi fedha hizo zinatumikaje.

Pia watoto wanalazimishwa kwa viboko kutoa fedha za kwenda safari za michezo mfano juzi mwanafunzi alipaswa kuchangia Tsh 2500 kutoka Nkuhungu kwenda mjini shule ya sekondari Dodoma, nilimpatia mtoto sh 1000 lakini aliadhibiwa nakutakiwa jambo ambalo kwetu sisi wazazi sio sawa kabisa nauli ya daladala ni sh 500 kwa watu wazima lakini tunapaswa kuwalipia sh 2500.

Vile vile kulazimishwa kwenda Kambi kwa kutoa shilingi 100,000 kwa mwezi wakati Kambi ni wiki 3 kwa uhalisia.

Vile vile baadhi ya Walimu wamekuwa wakilazimisha watoto kulipa hela kati ya sh 200 Hadi 1,000 pale wanaposhindwa kujibu maswali darasani.

Tunaomba Serikali iweze kufuatilia.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Majaliwa: Michango ya ovyo ovyo shuleni ambayo haina maelezo ikome
 
Back
Top Bottom