Kukodisha gari Tours

Kukodisha gari Tours

socialife

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
219
Reaction score
99
Naombeni mnipatie ushauri. Nimewakodisha Prado kampuni ya Travel Partner, wao wanaazimaga magari ya watu kwa kuwa hawana magari ya kutosha kukidhi mahitaji ya wateja wao. Baada ya kunisumbua sana kulipa, nilipitia mkataba nikagundua hauna clause inayoeleza kwamba watakuwa wananilipa kila mwezi.

Gari wamelitumia kwa miezi sita na kila siku ni 100k lakini wamenilipa ml 5 tu kwa kuwafuatilia sana na nimewanyanganya baada ya kukaa nalo bila kunilipa hata senti 1 kwa miezi yote 6. Mmiliki wa hii kampuni ni muhuni, wateja wake wanamlipa lakini yeye anaona taabu kunilipa mimi kama mteja wake. Nimegundua siko peke yangu ninayefanyiwa uhuni huu. Naombeni ushauri wenu nifanyeje nipate hela yangu.
 
Mkuu iko wazi hiyo unastahiki kulipwa ,fungua madai,kingine mlikubaliana hilo gari walitumie kwa muda gani? maana hapo umeorodhesha term of payment 100k/day na wameshalitumia kwa 6months.au ulikuwa ni mkataba wa kudumu mpaka gari life uwapelekee lingine?
 
Haha bro. wangu walisha mliza.
Walikodi haice miezi kadhaa walilipa kiwango kidogo sana ambacho sio makubaliano baadae tukakatisha mkataba.
 
Mkuu iko wazi hiyo unastahiki kulipwa ,fungua madai,kingine mlikubaliana hilo gari walitumie kwa muda gani? maana hapo umeorodhesha term of payment 100k/day na wameshalitumia kwa 6months.au ulikuwa ni mkataba wa kudumu mpaka gari life uwapelekee lingine?

Mkataba ni kuwa as long as wanalo wao.
 
Back
Top Bottom