Ngoja nikusaidie...
Kuhusu maharage ni kweli Kilindi kunafaa sana
Kuhusu mahindi pia ni kweli Kilindi kunafaa lakini si sawa na maharage
Kuhusu gharama;
[emoji979]Kukodi shamba ni elfu 30-40 kwa heka (mwaka huu ilikuwa 40)
[emoji979]Trekta inalima kwa elfu 30-40 heka, (mwaka huu ilikuwa 40)
[emoji979]Wapiga mashimo heka wanafanya elfu 15-20 (mwaka huu walifanya 20)
[emoji979]Wapandaji wanatoza elfu 5-10 kwa heka (mwaka huu watu wameshikwa elfu 10)
[emoji979]Bei ya gunia ni sh laki 2 na nusu njano (kopo 100 ndio gunia ambapo kopo ni kikombe fulani cha bati/rangi kinajazwa mpaka mlima- hawatumii kilo)
[emoji979]Mahindi kwa sasa gunia ni elfu 75 na kwa maeneo ya bara ni mpaka elfu 95 (gunia la mahindi kwa bara ni debe sita yaani ndoo kubwa iliyojazwa mpaka msonge/mlima-hawanaga mambo ya kilo)
[emoji979]Mahindi (kulima) ni kama nilivyoelezea hapo juu maharage ila yenyewe yanapungua gharama kwakuwa wanapanda kwa kutupia mbegu moja kwa moja wakati trekta inalima
[emoji979]Kuhusu maeneo kama nimekuelewa swali lako basi ni kwamba ukitaka kulima maharage chagua maeneo mawili tofauti yenye hali ya hewa tofauti (hiyohiyo Kilindi kuna sehemu wanaita NGULU/NGUU yenyewe orijino na kuna sehemu wanaita BARA)
[emoji979]Maeneo ya Nguu ya Bara ni kama vile maeneo ya mpakani na Kiteto mfano Baina, Kibrashi, KwaLebali, Kweditinga, Songe kwa upande wa Magharibi
[emoji979]Maeneo ya Nguu isiyo ya Bara yanayotoa Maharage ni kama vile Nkalanga, Chala, Huyaga, Sakandala, Kwedisasu
[emoji979]Mahindi yenyewe yanakubali sana maeneo ya bara kwenye matambarare (Kwa wao unaposema bara ni Kilindi ya mpakani upande wa Magharibi, Kiteto yote, baadhi ya maeneo ya Morogoro, maeneo ya Dodoma na sehemu zinazofuata kuelekea Magharibi)
[emoji979]Mambo mengine sijafafanua kwakuwa umesema wewe ni mkulima utakuwa unaelewa moja kwa moja. Mfano swala la maharage kwa mashamba ya upande mwingine wanawahi kuvuna na wengine wanachelewa... kadhalika mahindi kule bara wanapanda mara moja tu (dec/jan/feb) wakati upande ule mwingine wanapanda hata mara mbili (sept/oct/nov na dec/jan/feb)
[emoji979]Maharage kwa asilimia kubwa kilimo kinachanganyia mwezi February (yaani mwezi wa pili ndio wengi wanapanda)
[emoji979]Nimeeelezea zaidi kwa kubase maeneo ya Songe, Mafisa, Kibrashi...na Gombero kwa mbaali kwasababu ndio maeneo niliyo na uzoefu nayo
Nadhani nimejitahidi kufafanua kama kuna swali uliza... Swala la uchawi alilosema mjumbe hapo ni upuuzi tupu halina mashiko yoyote wewe nenda kapambane!