Kukojoa mara kwa mara kunatokana na nini?

Joined
Sep 20, 2007
Posts
69
Reaction score
2
Jamani tatizo langu ni kukojoa mara kwa mara ninapokunywa kimiminika chochote. Hali hii hunikosesha raha maana kama nina mkutano inabidi nisinywe chai wala maja.

Kitendo cha kunywa glass moja ya maji au kikombe cha chai kinanifanya nihudhurie maliwatoni kila baada ya dk 7 hadi 10 mara 3 au 4 ndo nakuwa sawa.

Nikinywa bia hali ndio inakuwa mbaya zaidi... Hali hii inaninyima raha sana. Je ni tatizo gani na nifanye nini?

==

==

=====

 
Ndugu yangu Mpiganaji..

Kabla hujamtafuta mchawi wako nenda kapime Kisukari. Hizo ni dalili tosha za kisukari; Kama huna kisukari basi njoo tena hapa utuambie level ya sukari yako ni ngapi kwenye mwili wako ndipo tuendelee na mangine.

Njimba
 
Hapo unaweza kua na kisukari au maambukizi ya njia ya mkojo.Pima mkojo na utajua ni lipi kati ya haya
 
Nilisha enda hospitali nikapima, blood sugar iko normal na mkojo pia ukawa safi. Daktari akanipa madawa fulani nitumie, nikamaliza lakini hali ikawa hivyo hivyo. Majibu ya hospitali siko zote yamekuwa sina tatizo. Lakini mimi nikijilinganisha na watu wengine naona nina tatizo. Au kibofu kangu cha mkojo kidogo nini, te he he he.
 

Umejaribu kucheck prostate cancer? Kukojoakojoa mara kwa mara ni dalili ya prostate cancer pia. Kama ujacheck ningakushauri ufanye hivyo.
 
Kukojowa Mara kwa Mara pia kunasababishwa na Mawazo jaribu pia kupnguza mawazo uliyokuwa nayo kichwani mwako mimi pia nina matatizo hayo ya kukojowa kila mara haswa nikinywa chai au maji ya moto huwa nakwenda ****** kila wakati na nimekwenda kupima kwa Doctor kasema sina ugonjwa wowote najaribu kupunguza kunywa chai na maji ya moto na Mawazo pia ndio Dawa yake hakuna Dawa ingine.
 
Hivi ni kipi kinachosababisha watu wenye kisukari kukojoa mara kwa mara?
Na je kuna kitu kingne kinaweza kusababisha hali hiyo?
 
Wanajamvi mko salama na mnaendelea na ujenzi wa taifa letu?

Kama Kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni kwamba karibu ni mwezi mzima sasa nimekùwa nikisumbuliwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara inafikia kiasi ndani ya saa moja nakuwa nimekwenda kukojoa zaidi ya mara mbili na Mkojo unakuwa zaidi ya nusu lita kila ninapokwenda kukojoa.

PIA kwa siku huwa nakunywa maji lita 3 hadi 4.

KIKUBWA NINACHOWAOMBA WAKUU NI KUTAKA KUFAHAMU KAMA HILI NI TATIZO GANI NA PIA USHAURI WENU JUU YA HILI TATIZO.

Ninatanguliza shukran kwa Msaada wenu. +ME
 
chek sukari mkuu, ila ngoja waje wataalam watakujuza!
 
Pole sana. Na je, maji unakunywa sana? Nenda hosp watashauri zaidi inawezekana ni diabetes kama walivyo hisi watangulizi
 
Mkuu wala huna tatizo kabisa,Tatizo pekee ni kwamba unakunywa maji mengi sana hata kama huna kiu hapo lazima utakojoa mara kwa mara wala sio ugonjwa mkuu,punguza kunywa maji mengi kupita kiasi
 
Huna Tatizo
Hata Mimi Nakunywa Maji Lt 5 Kwa Siku
Nakojoa Lt Moja Na Nusu Kila Baada Ya Masaa 5
Nishazoea Kwani Nina Miaka Mitano Ktk Unywaji Wa Maji!
 

Ndugu hilo ctatizo bal ni maji unayokunya ni mengi naunajua maji yanasharabiwa tumbon na kama unasikia kiu mara kwa mara ctahid kuchanganya maji na chumvi au sukar ilkufanya usharabiwaji kuwa kwa kiasi kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…