Onaa, kukojoa sana inategemea;
0. Muundo wa kibaiolojia wa miili yenu, wembamba saana, hukojoa sana, yaani hawa jamaa hawajui kabisa 'uchumi' wa maji. Pia saizi ya kibofu maana kama tu matumbo yanavyotofautiana. Na vibofu vilevile madam.
1. Tabia zenu za unywaji maji kama familia. Mfano kwetu tushaigana kila mmoja akiamka tu anakunywa maji, tofauti na familia nyingine ambapo wao wameigana kunywa maji hadi iwe kiu.
2. Tabia ya kuona kuwa kukojoa usiku sio ajabu, kama familia
Pia na mambo mengine huchangia mfano:
Jotoridi la eneo unalokaa, kama ni baridi usiku utajikuta unaamka sana kukojoa, kama ni joto hautaamka sana (au hautaamka kabisa)
So kwa kusema hayo una mawili unaweza kufanya:
1. Kuhamia mazingira yenye joto, ili utoe jasho zaidi badala ya kutegemea mkojo
2. Kubadili ufikiri na tabia ambako kutachukua hatua tatu au nne;
i. Hatua ya sasa, hatua ya sifuri ni
self indulgence: yaani mwili wako unakiamrisha kukojoa muda wowote unaoutaka nawe unatii. Almost no controll
ii. Hatua inayofuatia ni
self discpline, kwako ww ndo hatua ya kwanza. Tafuta kufanya kwa kujirudia (ikibidi kujilazimisha) kufanya matendo ambayo yakijumlishwa yanapelekea usikojoe saana usiku. Wameshauri wadau suala la kudhibiti muda wa kunywa maji, Mazoezi nk
iii. Baada ya hapo utafikia
self control, hapa mwili utaanza kukuelewa na kuitikia ipasavyo. Hata ukiishia hapa inatosha kabisa.
iv. Hatua ya mwisho na ya nyongeza ni
self mastery. Ambapo unaweza kuuamurisha kabisa mwili wako kwamba utumie mbinu nyingine(labda jasho, au kuconvert to uric acid) lakini usikusumbue kukojoa usiku. Hatua hii ni ya kitata zaidi. Self mastery ni nomaa😱
Nimeandika kwa kirefu kama msaada, hizi ni hatua mtu yeyote anaweza kupitia kurekebisha tabia yoyote, ama kuiacha au kuianza. Inaanza tu na NIDHAMU BINAFSI, SELF DISCPLINE💪