Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Tumekua tukishuhudia utekaji wa watu nchini vikifanywa na eti wasiojulikana! Hawa wasiojulikana ni watanzania ambao huenda wamejiambatanisha na vyama vya siasa, hata hivyo ni CCM tu ndiyo ina vikundi vinavyojulikana kama Chawa, Uhamasishaji, Wadudu na Green Guard(Umoja wa vijana), hawa huenda wanaweza kuwa wanatumia kauli ya ukinizingua chawa wangu hawatakubali, na tukiangalia utekaji unawakumba mashabiki wa upinzani zaidi kuliko wa CCM.
Kutokana na nilivyoeleza ni vizuri Serikali ikapiga marufuku vikundi vyote hivi wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na wa Rais na Wabunge ambako kutazuka wimbi la vikundi vya ulinzi.