Kukopa sana na mfumuko wa bei vina uhusiano gani?

Kukopa sana na mfumuko wa bei vina uhusiano gani?

IQup

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2018
Posts
1,166
Reaction score
1,808
Haya maisha kadri mtu mmoja anavyozidi kukopa huko nje na kuleta pesa hizo humu ndani kumekuwa na mfumuko wa bei katika bidhaa nyingi sana. Yaani kila bidhaa masokoni madukani na popote bei imezidi kupanda kila wakati hadi kusababisha wananchi kuwa na maisha magumu kila kukicha. Hadi najiuliza kuna uhusiano gani kati ya kukopa sana na mfumuko wa bei?

Nimekumbuka hayati Magufuri hakuwa akikopa sana na hata akikopa pengine ilikuwa haitangazwi kama sasa, uzuri bei ya bidhaa nyingi ilikuwa ikishuka, je huyu tuliyenaye nani anayemsaliti hadi maisha yawe yanazidi kuwa magumu kila kukicha na bidhaa kuzidi kuongezeka bei zake?

SWALI: Kwanini wanawake walio wengi wanaamini katika KUKOPA, KUPEWA BURE, ama kupenda kusafiri sana na kupenda sherehe za hapa na pale? Huku mtaani kwetu naona wanawake hupenda sana kukopa kila mahali lakini hawafanikiwi kimaisha, wanapenda kupewa bure kila waonapo fursa, wanapenda safari ambazo zingine hazina umuhimu wala maslahi, hivyo hivyo hupenda kuweka sherehe hadi matukio ambayo si ya muhimu.

KITAIFA nimehisi mambo kadhaa kutoka kwa kichwa changu:

Kuna kakikundi kanamhujumu Rais wetu; kila tukio wanataka washerehekee ili wajilipe posho na kujilipia safari za kusafiri washinde na matukio muda wote ili wazidi kupata pesa za safari na miposho. Pesa zinakopwa lakini matumizi mengine yanakuwa si ya kimaendeleo, hii hali tulishaanza kuisahau ila naona kuna watu wanamshauri mama aone hayo matukio yanaumuhimu uwaruhusu kuyafanya..mwisho pesa za mikopo zinazidi kutumika kujilipa tu.

WAKATI MWINGINE KUKOPA SANA SI KUFANIKISHA KULETA MAENDELEO, Ona watanzania kila siku tunalia bei kupanda kwa kila bidhaa kila wakati kilio, kwanini mheshimiwa asijikite sana kudhibiti mifumuko ya bei katika bidhaa kuliko kuwa bize kukopa hizo pesa??. Wananchi tunateseka sana huku chini, hizi bei zinaongezeka kila wakati zinatutesa kwakweli.

Mheshimiwa Rais na genge la karibu yako muda mfupi mtaanza kuuwa wananchi maana maisha yanazidi magumu sana. Wananchi hata tukichanja watu wote ila kama tunashindwa kununua chakula sababu ya bei kuwa kubwa mjue chanjo hazitasaidia kuokoa lolote, acheni kupiga porojo za chanjo mjikite kudhibiti mifumuko ya bei katika bidhaa.

Nawatakieni heri ya mwaka mpya 2022! CCM na serikali kuweni makini mtaua wananchi wenu, oneni mifumuko ya bei katika bidhaa
 
Shida hawapo kwaajili ya wananchi..wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao, usitegemee la maana kutoka kwao.

Wanatapanya mali walizokopea kwajina la wananchi wa lipa kodi.

Katiba mpya ni hitaji la wananchi

Mungu ibariki Tanganyika

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom