Kukosa hamu ya kula kwa mtoto

Kukosa hamu ya kula kwa mtoto

Inawezekana anakula chakula kinachomtosha lakini kwa macho yako unaona hana hamu ya kula, ukumbuke tumbo la mtoto si kubwa sana. Hao wanaitwa fussy eaters wanasumbua. Jaribu kumwekea chakula ambacho akisikia njaa anakuja kupick na kuondoka, kama karrots, vipande vichache vya nyama vikavu, matunda n.k.
 
Jitahidi pia kubadilisha aina ya chakula chake ila zingatia kumpa kile chakula kinachoendana na umri wake Kama ana miezi zaidi ya sita apewe hata supu za maharage yalichemshwa kidogo juice za matunda fresh prepared at home nakadhalika sio uji na maziwa tuu asubuhi , mchana na jioni lazima apoteze hamu ya kula fastaaa
 
Pia kula na watoto wenzake inaweza kusaidia wanasema social interaction inabadilisha watoto kuanzia kuongea, hata kula.
 
Ana upungufu wa Vitamin B complex. Nenda famasi wakupe dawa ya Vitamin B. Pamoja na hilo mpe sana juice za matunda chachu kama machungwa, mananasi n.k
Juice ziwe za kutengenezwa nyumbani. Sio zile za kwenye mabox.
 
Back
Top Bottom