Kukosa Hela

Kukosa Hela

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Najisikia kuumwa sio kuumwa. Nasikia baridi, koo limekua kavu, najaribu kulala usingizi hauji, najisikia kama nikae chini nilie halafu nikiwaza kuna watu nawadai hela zangu na mpango wa kunipa hata 100 hawana natamani ningekua na nguvu niwakamate niwapige. Niombeeni na mimi leo mipango yangu ya hela ikae sawa maana mnaweza nipoteza hii hali ikidumu kwa siku mbili tu.
 
Duh!...siku hizi kukosa pesa ni suala la kawaida sana.

Mimi binafsi mwezi ulioisha hali yangu kifedha ilikuwa mbaya lkn namshukuru mungu tokea tarehe 24 mambo yangu yamerejea pale napopataka

Mungu akufanyie wepesi upate mtu akukopeshe hata kidogo naww
 
Bora Wewe uliyekosa tu Hela Mkuu kwani mwenzako Mimi nimekosa Hela, Mbunye na hata Kipaji changu cha Kutongoza nacho siku hizi Kimetoweka kabisa kwenda Kusikojulikana hivyo mambo kuwa ' valuvalu ' tupu.
 
Asante mkuu. Mimi huyu mdeni wangu mmoja mpaka rb nimemkatia anaitwa polisi haendi. Ila week hii atajifunza.
Wanakera sana watu wa hivi, wamenifanya nijifunze kutokopesha mtu hata awe na shida gani
 
Najisikia kuumwa sio kuumwa. Nasikia baridi, koo limekua kavu, najaribu kulala usingizi hauji, najisikia kama nikae chini nilie halafu nikiwaza kuna watu nawadai hela zangu na mpango wa kunipa hata 100 hawana natamani ningekua na nguvu niwakamate niwapige. Niombeeni na mimi leo mipango yangu ya hela ikae sawa maana mnaweza nipoteza hii hali ikidumu kwa siku mbili tu.
Sawa Nitafute....
 
Aisee yaani siku hizi kudai pesa yako ni kama ugomvi vile. Mm kuna watu kama wanne hivi ninawadai lakini cha kushangaza ni pale ninapo itajia kiasi changu hawanipi kila siku napigwa kalenda tu. Yaani isha kuwa kama ugomvi mpaka nisha kausha tu wakinipa sawa na wasipo nipa sawa tu.
 
POLE SANA MKUU ZAMA HIZI SIO ZA KUKOPESHA WATU ,UNAWEZA KUONA WATU WABAYA BURE KUMBE VYUMBA
 
Duh!...siku hizi kukosa pesa ni suala la kawaida sana.

Mimi binafsi mwezi ulioisha hali yangu kifedha ilikuwa mbaya lkn namshukuru mungu tokea tarehe 24 mambo yangu yamerejea pale napopataka

Mungu akufanyie wepesi upate mtu akukopeshe hata kidogo naww
Kukosa hela hakuzoeleki mkuu. Hasa ule wakati una jambo unataka kulifanya na pesa hamna. Ameen mkuu ila sitaki wa kunikopesha naogopa sana madeni
 
Nilishawahi kumfuata mtumishi mmoja nikamkate hata panga maana nilimdai miaka miwili bila majibu.
Bahati nzuri sikumkuta ningemkata hasa kwa usumbufu alionipa
 
Bora Wewe uliyekosa tu Hela Mkuu kwani mwenzako Mimi nimekosa Hela, Mbunye na hata Kipaji changu cha Kutongoza nacho siku hizi Kimetoweka kabisa kwenda Kusikojulikana hivyo mambo kuwa ' valuvalu ' tupu.
Kama huna hela unapata wapi nguvu za kutongoza. Hayo yote ni matatizo ya kukosa hela mkuu
 
Back
Top Bottom