kukosa mikopo ya elimu ya juu, majibu tunayo wenyewe.

beneli

Member
Joined
May 1, 2013
Posts
86
Reaction score
7
Habari wanajukwaa ,poleni kwa mahangaiko ya kupata elimu maana mwatimiza maagizo ya muumba yeye aliyesema uza mali ukapate ufahamu..moyo wangu wauma hasa kwa kuona wasomi wengi wakiumia kwa kukosa ufadhili wa bodi ya mikopo ,wengi wakiwa wamekata tamaa na elimu kwa ujumla., wengi tunajua elimu sio mteremko na tumepitia mengi hadi kufikia sasa, wasomi wengi wa maswala ya fedha ,uongozi na sera wamesoma kwa mikopo hii hii na ni aibu kwa wasomi ambao wanatakiwa kuishauri serikali wao pia kulalamika, natumai wengi tunapenda kuona wadogo zetu wakisoma kwa amani miaka ijayo na kwa hivyo ningewashauri wataalamu wa fani mbalimbali kama maswala ya fedha(finance) uongozi wa biashara(bba) takwimu na uchumi , wakae pamoja na kutengeneza mpango (financing plan) utakao wasilishwa serikalini utakao husu namna ya kugawa mikopo kwa usawa utakao wafaidisha wanafunzi wote wenye uhitaji ,kuanzia na ada za vyuo, malazi na makazi pamoja na vyakula vitu vinavyotutesa wanafunzi wengi. Naweza onekana kama mwanasiasa ila ninachojaribu kusema ni kuwa sijawahi ona wanafunzi waliohitimu wakijaribu kutatua tatizo hili zaidi ya kulaumu na kukimbia kulipa madeni yao.nadhani imefika wakati sisi sisi wenyewe tuwe sehemu ya kutatua tatizo..elimu yako haina maana kwetu kama haitatukomboa..Nawasilisha.
 
Kiukweli roho inaniuma nkiwa kati ya walio not secured kiukweli naumia sana yan nimeshakata tamaa maana maisha ni magumu
 
nakumbuka miaka ya 2003 nikiwa 2nd yr pale udsm wkt tunapambana kuondelewa kwa huu mzimu wa bodi ya mikopo
sintasahau yaliyonikuta mbaya zaidi jamii haikutuunga mkono sasa wacha
kila mtu aonje joto la jiwe.
 
Ni kweli kabisa mkuu,
yawezeka tulisoma zamani tena kwa ufadhili wa heslb,
tunapowaona madogo wanahangaikia haya maswala, tunapiga kimya as if we're not concerned,
tunasahau kuwa hawa ni wadogo zetu,ambao nao wana ndoto za kutengeneza kesho yao,
still hatukumbuki kuwa hapo baadae tutahitaji kusomesha watoto zetu hapo ,
ili kuandaa system nzuri ktk hili ni jukumu letu sote kuweka mambo sawa....

Swali linakuja hapa;
Ni kivipi tunaweza kufikia hicho tunachokitarajia, wakati kila kitu kimeshaoza serikalini...
 

tukiweka vichwa chini na kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa tutafanikisha 'if u want something be done right , do it uaself' swala la kujifunza namna bora ya kuendesha bodi haliwezi likaachiwa watu wachache wa bodi waende study tour ya wiki moja then u expect waje na best option ,no! Tuna nguvu ya teknolojia siku hizi na elimu inapatikana kila mahali , kwanini hamna hata study moja ya kuforecast uhitaji ? Uwezo wa bodi ? Vyanzo vya mapato ? na vyanzo vinavyoweza kufinance bodi kwa ujumla,..ifike mahala tuhoji with facts na kutoa solution ya kudumu ,maana next year ongezeko litakuwa kubwa kuliko hata mwaka huu..i guarantee u that.
 
Kama wanaharakati tumejitahd kufatilia suala hl tangu mwanzo,kuanzia Bodi ya mikopo,wizara ya elimu,kwa Waziri mkuu,kwa Baba RIZ ila huko kote hatukpata msaada na majibu yenye tija,tumeamua kwenda MAKAO MAKUU CHADEMA,tumekutana na wakubwa akiwemo Mweshimiwa Myika,tumepewa ushauri kuwa jumanne tarehe 15,kamati za bunge zinaanza,tunatakiwa kuwepo pale posta BUNGE DOGO hasubuhi saa tatu tutakutana na WABUNGE wengne ili mchakato huu ujadiliwe kitaifaUpyaa,hvyo kama upo hapa dar au mkoani na kuna mtu anamfahamu tafadhali mwabalishe, tumeambiwa wingi wetu ndo utachangia suala hili kuonekana lina mashiko na kupatiwa suluhsho sio maswala ya KASUNGURA KADOGO. tufahamishane kwa pamoja linawezekana.NAWASILISHA
 

1 Like
 


Yaani ni sawa na ile "hadithi ya tumfungaje paka kengele"....

Ni kweli kabisa tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu waliopiga hatua, tunaweza kuandaa watendaji wazuri wa bodi ,tunaweza improve techno. tunaweza kuifinance bodi fungu kubwa...

Tatizo linakuja hapa:
How can we oversee board's (servants/agents/officer) ethics?
 

we can even suggest the structure of the board itself...ndo maana nikaweka na wataalam wa mambo ya uongozi wahusike.
 
Swala ni kwamba watu ambao wamepewa nafasinya kusimamia elimu,,,ni watu ambao wanastaili kusimamia ujenzi wa vyoo,,,maana kama kiongozi anatambua umuhimu wa elimu,,awezi kutoa majibu ya ovyioovyio,,kama wanayotoa wafanyakazi wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu,,,,unakuja pale bodi,,,mfanyakazi wa bodi anakuuliza,,,''umekuja kufanya nini?umekosa mkopo?nenda kwa mkuu wa nchi''.haya maneno yanatamkwa kabla wewe ujaeleza shida yako,,,ni kweli hi nchi ni ya kwetu sote?au ya watu fulani?
 
Kilichobaki sasa nikuunga mkono tamko la CDM kwenda makao madogo ya Bunge.

Shida hapa ni kwamba watajitokeza wachache na wengine kubaki nyumbani kusubiri feedback. Hiyo sio poa.

Waliopata mkopo pia wakiwa na nafasi wajitokeze. Najua wengi watashindwa kutokana na kufunguliwa kwa vyuo.

Mimi nitajitahidi niwepo na nitahamasisha vijana wengi ambao naamini hizi habari hazijawafikia.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
nakumbuka miaka ya 2003 nikiwa 2nd yr pale udsm wkt tunapambana kuondelewa kwa huu mzimu wa bodi ya mikopo
sintasahau yaliyonikuta mbaya zaidi jamii haikutuunga mkono sasa wacha
kila mtu aonje joto la jiwe.

Selfish!!.. brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…