Da Vincis Code
Member
- Jul 21, 2021
- 15
- 20
Mnamo tarehe 30/Jan/2021 Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liliteua tume ya kusimamia uchaguzi wa Shirikisho la Riadha Tanzania. Tume ilikua chini ya uenyekiti wa Dr Jonas Tiboroah japo mchakato huu ulifanywa na BMT kwa nia njema ya kurudisha utawala bora katika chama, bahati mbaya sana tume hii ilikosa umakini na kupelekea kuchaguliwa watu wasio na sifa hali ambayo kwasasa inaleta usumbufu mkubwa kwa Shirikisho hilo.
Mpaka sasa viongozi wawili wa RT wameshajiuzulu japokua barua zao za kujiudhulu zinatoa sababu binafsi, lakini inafahamika kua sababu halisi ni msukumo uliotokana na viongozi hawa kukosa sifa za kushika nafasi hizo.
Hivi karibuni tumeshuhudia Makamu wa Rais wa Shirikisho ndugu John Bayo akijiuzulu kwa kutoa sababu kuwa miradi yake inakufa kwakuwa hana muda wa kutosha kuisimamia kwakuwa muda mwingi anautumia kwenye shughuli za riadha.
Hata hivyo, kujiudhulu kwa ndugu Bayo kumekuja wakati kukiwa na kelele nyingi sana zilizodai kuwa ndugu huyu hakuwahi hata kumaliza kidato cha nne achilia mbali kukosa elimu ya Diploma inayotakiwa kwa nafasi ya Makamu wa Rais wa RT.
Sasa baada ya Bayo kutoka kwa hiari yake bado jinamizi la kughushi vyeti halijaiacha RT na hii ni muendelezo wa kukosa umakini kwa tume ya Dr Tiboroah, Mjumbe wa Kanda ya Ziwa, Ndugu Donald Ramadhan Machibya naye anatuhumiwa kuwa ameghushi cheti cha mafunzo ya ualimu wa Riadha ili aweze kupata sifa ya kugombea nafasi hiyo. Ndugu Machibya ameghushi cheti na kughushi na sahihi ya Mh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ndugu Anthony Mtaka hali ambayo inamnyima sifa za moja kwa moja za kuwa kiongozi kwa kutenda kosa la jinai, lakin pia inamfanya akose sifa za kikatiba za kushika nafasi alionayo.
Habari za uhakika zinaeleza kuwa ndugu Machibya alighushi cheti hicho kwa kutoa nakala ya Mwalimu wa riadha wa mjini Geita (Jina linahifadhiwa) na kufanikiwa kuibandika sahihi ya Mhe Mtaka.
Napenda kushauri viongozi wa RT waliopo madarakani hasa Rais wake wakili Silas Isangi asifumbie macho swala hili kama anataka taaisis anayoisimamia kuwa na taswira nzuri kwa jamii.