Kukosea kuwekewa float kwenye namba ya wakala

Aureus Ndimbo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
211
Reaction score
95
Jamani Mimi ni wakala mdogo wa airtel money.sasa Kuna hela imeingia lakin cjaona msg ila hela ipo. Sasa jamaa anafanyia kazi Airtel makao makuu wilaya amekuja ameniambia Kuna hela imeingizwa kwenye laini yako km float kimakosa hivo irudishe,na msg ya lain iiliyotuma pesa hajanionyesha.Nimemkatalia nimemuambia awasiliane na huduma kwa wateja wairudishe wenyewe.lkn amenitishia kwenda kufunga lain yangu.ipoje hapo nafanyeje
 
Mwizi tu huyo,endelea na musimamo huohuo ukikubali matakwa yake imekula kwako, halafu kama ni wakala wa airtel kweli mtolee taarifa makao makuu ya airtel.
 
Tapeli huyo..jichanganye walambe yote ubaki na laini tupu
 
Ume request Salio ukaona kweli ipo? Kama ndio Mwambie airudishe mwenyewe huko aliko
 
Kwanza huyo mtu aliyekuja wewe unamfahamu na una uhakika Kama ni kweli ni mfanyakazi wa Airtel?Kama humjui ila yeye ndio amejinadi hvyo basi ujue ni tapeli huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…