Kibingu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2022
- 1,078
- 1,445
Hayati John Pombe Magufuli, aliukuta mchakato wa katiba mpya umefika mahali pazuri pa kupigiwa kura.
Hayati Magufuli akazipuuza harakati za miaka nenda rudi za waTanzania zilizolenga kuipata katiba mpya.
Magufuli kwa kiburi na jeuri akasema kutengeneza katiba nzuri itakayowapa mwangaza mpya wa karne zijazo watanzania ni upuuzi.
Magufuli akawaamrisha watu wakafanye kazi za kutumia nguvu za mwili pekee, nasisitiza na wasijaribu kutumia akili kufikiri wala kuwaza mambo mapya.
Akawaaminisha watanzania kuwa ni yeye tu anayejua mahitaji ya watanzania. Akaamrisha anayewaza kinyume auliwe kisha asongezwe kwenye viroba akatupwe.
Unyama mkubwa aliufanya lengo aweze kusimika utawala wa mawazo yake pekee, kinyume na matakwa ya watanzania.
Kwa bahati mbaya sana masalia ya umagufuli bado yanatembelea zile kauli zake kuwa eti watanzania hawapaswi kuwaza lolote kuhusu mustakabali wao hasa kuhusu katiba, demokrasia na haki za watanzania kwa ujumla wao.
Masalia haya, yatachukua muda kuyaangamiza kikamilifu. Awamu ya sita inataka kuyaondoa lakini inasitasita.
Lakini ni wazi kuwa, kutokuwepo kwa katiba mpya Tanzania kwa kipindi chochote kuanzia sasa, na madhara yake yoyote, yawe ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na hata amani na utulivu wa nchi, lawama zitaenda kikamilifu kwa huyu hayati aliyejiita jiwe,John Pombe Magufuli.
Nawasilisha, tujadili.