Shule za advance zilifunguliwa July 1 2024 na tukapewa maelekezo ya kutumia mtaala ulioboreshwa.
Tukapeenda na seminar zilizochukua takriban siku 3, kutoka mtaala uliopita kuna masomo yalifutwa kama General studies(GS), na kuna yaliyobadilishwa kama Commerce kwenda business studies, kuna yaliyoongezwa kama Historia ya Tz na maadili na Academic communication, na kuna combi ambazo awali hazikuwepo ila sasa zipo na kuna wanafunzi wamekuja mashuleni kwa masomo hayo.
Sasa ni mwisho wa mwezi, tunapokea taarifa za kurudi kwenye mtaala uliopita sababu zikiwa kukosekana kwa vitabu. Hawakuliona hili kabla ya agizo la kuutekeleza? Umepotea muda, na pesa nyingi sana kwenye zile seminar.
Kikubwa zaidi, jamani tunawachanganya sana wanafunzi. Na kuhusu hizi combi mpya, mbona hatupewi utaratibu?