Mbute na chai
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 564
- 593
Ndugu, rafiki, na jamaa Jforums, poleni sana hasa wanafunzi wanaongoja kwa hamu kujua kama wamepata mikopo toka HESLB. Ukimwa wa HESLB ni dharau ambayo taasisi nyingi zenye dhamana za serikali huwa nayo. Ni wazi kuwa mgawanyo wa fedha huitaji umakini, lakini umakini huu pasina taarifa ya hatua zilizofikiwa ni umakini gani? Serikali iliyo wazi, uwazi wake hujidhihirisha kupitia upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya kinachojiri katika utendaji kazi wake. Dharau hii imejidhihirisha pale wanafunzi wanapoomba taarifa toka HESLB, kwani ni haki yao, na kupewa majibu ambayo ni ya mtu kujisikia (discretionary), yanayopelekea baadhi ya wanachama wa jf kuweka mada juu ya HESLB zilizowafanya waonekane waongo. Kwasababu hii, bodi ya mikopo elimu ya juu imepewa madaraka ya kupitiliza, hivyo ni wakati sasa serikali ipitie upya madaraka haya na kuweka mda maalum wa wanafunzi kutuma na kupata taarifa ya maombi ya mikopo. Na hii huonesha umaskini wa utumiaji wa elimu tunayoipata kwa manufa yetu na vizazi vijavyo kwani wafanyayo haya ni wasomi tena wenye shahada za uzamivu n.k. Tafadhali bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu toeni taarifa mmefikia wapi kwani baadhi ya vyuo huanza usajili juma lijalo mwezi huu wa tisa.