Ndugu,nijuavyo mimi ni kuwa hawatakaa wagundue tatizo kirahisi. Pia naona kidogo haukutaka kuwa mkweli kwani kama ungekuwa unapeleka physically ndo mtu angekwambia ivo lakini kwa kujua tu index number bila hata jina tayari wanajua jina likoje.
Nakushauri urejiste kwa kutumia majina yaliyo kwenye cheti cha form4, baadae ukaombe kubadili iyo karatasi.
Ikumbukwe result slip si cheti, kwa iyo mpaka cheti kinatoka iyo result slip itakuwa inaexpire na jina la cheti litakuwa lile uliloandika wakati unajiandikisha kufanya mtihani.
Usihofu maana matokeo ya f4 ndo yaliyokupeleka fom5 kwa iyo baraza wana jina lako sahihi. Cha muhimu maelezo yako yote uyaweke ktk jina la fom4 na ndo cheti kinachofanywa reference kwa mkopo, kwa miaka yote ukaayo chuoni.
Ndugu ukianza kujichanganya na kuwaeleza wanaoandikisha mfano mkopo n.k utajikwamisha. Ukisha apply,nenda baraza la mitihani upate kopi nyingine.
Kuna mchangiaji kasema vyeti hutumia miezi6, ila nadhani tatizo lako ni results slip, ambayo ndani ya siku1 au2 unaipata pale baraza.
Note:
Kama ukiangalia matokeo yako ya f6 ktk website ukakuta jina limekosewa ujue hata cheti kitakuja kwa jina ilo,ila ukiangalia moe web,au necta website ukakuta jina liko sawa, basi tulia usubiri cheti chako.
Ni ushauri wangu tu, na nakutakia mafanikio ila usipaniki kwa tatizo ilo mdogo wangu.