Kuku aina ya kuroiler from India

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Wakuu kwa mara nyingine nimefanikiwa kuagiza hawa vifaranga wa Kuroiler. Hawa ni kuku kutoka India na wanaweza fugwa free range na hawa like Dorep wanakuwa wakubwa sana. So by mwezi wa 12 nitaanza kutoa supply ya kwanza ya hawa kuku.

=============================================

 
Haya ngoja ifike hiyo December maana nasikia hata Uganda wapo ila tunasubiri bei yako maana hujasema upo wapi labda Bukoba na umesema umewapata kutoka india
Tupe angalau bei ya kuanzia
 
Mkuu nime agiza F1 kuna kampuni moja ambayo inadili na kuagiza fertilized eggs na vifaranga kutoka nje ndo wameniagizia, na kuna moja naisubilia kutoka South Africa ni breed ambayo inataga mayai kama mvua.
Hao wa Uganda niliwaona ila sio wanechakachuliwa hata krnya kuna janaa anao ila nao kwa kweli wameisha chakachuliwa.

Kuku wa mbegu inatakiwa wawe F1 so utakuta mfano hawa tunao waita wa malawi kwa sasa si ni F 20
 
Kuhusu bei usijali ila hata mayai nitauza tu kama una mashine yako utaangua mwemyewe. Kuna watu huwa hawataki kabisa kuuxa fertilized eggs wao ni vifaranga tu. Ila mimi nitauza fertilized eggs za SASSO, KUROILER na wengineo
 
Safi sana mkuu Chasha..

Vipi kuhusu uzito wao ni Kg ngapi maana nakumbuka ile mbegu yako ya Kenya ulitoa data nyingi sana including uzito wa majogooo na matetea..

Tusubiri huo mwezi wa kumi na mbili tufanye membo..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hawa hufikia 5 kg ila moja ya sifa za hawa kuku unaweza wafuga free range na wakajitafutia wenyewe. Kwa uzito bado hawajafikia DOREP ambao ni 8ngapi kg, ila Dorep kuwafuga free range kidogo ni shughuri, ila hawa pamoja na SASSO unawafuga na wanaweza jitafutia wenyewe ingawa bado unatakiwa kuwapa chakula cha ziada na unaweza pia kuwafuga kama wa kisasa
 
kuna kuku huwa wanatumika india kuchezea kamari ama kupiganisha huku dar wanauzwa tsh 100,000 mmoja! wapi naweza pata kwa bei rahisi?
 
Mkuu hao ni wale wa fighting wanatumika kupiganisha na michezo ta kupiganisha kuku ni maalufu sana India, Pakstan,huko kwa Watalebani na kazalika, ni kama ilivyo kwa wale ng'ombe wa fight wanao pigana huko Spain na keingineko.
Mkuu hao kwa kweli sina na kwa huku bongo si dhani kama wana ishu sana
 

Mkuu hawa SASSO unauzaje bei ya kifaranga? na wanakuwa na umri gani?
 
Wakuu kwa mara nyingine nimefanikiwa kuagiza hawa vifaranga wa Kuroiler. Hawa ni kuku kutoka India na wanaweza fugwa free range na hawa like Dorep wanakuwa wakubwa sana. So by mwezi wa 12 nitaanza kutoa supply ya kwanza ya hawa kuku.

Umewatoa lndia moja kwa moja?
 
jaman kabla ya hao wa INDIA mm naomba ushari ni wapi nawezakupa kuku wa Malawi ambao ni mbegu bora kwa maana wanataga mayai vizuri!

Mkuu hawa kuku wa Malawi mpaka tulipo sasa inaweza kuwa ni kizazi cha hata 50 yaani F50, Na tangu wavushwe kutoka Malawi hadi Bongo ni muda sasa, na tatizo kubwa ni inbreeding,

Hivyo kama unataka mbegu bora ya Malawi yaani F1 ni lazima u cross wewe mwenyewe na hawa kuku si kweli kwamba wana asili ya malawi, ila lbda watu wa kwanza kuwachukua waliwachukua Malawi.

Austrolops,ndo kuku wa kuku cross upate hao wa Malawi inaw sijuia kwa Bongo ni wapi kuna hawa austrolops original kabisa kutoka Australia


Haw ndo Austrolop ambao walitumika ku cross na kupata hao kuku wa Malawi
 
nimekupata Mkubwa kweli hii ni mbegu ya maana, vp hiyo company unayosema inaagiza kutoka INDIA hawaagizi hawa kuku wa malawi, au hawa kuku wa malawi (weus) ma wale wekundu wanawaita (kuchi) wapi wanataga vzuri na hawasumbui kwa magonjwa! au ni kuku aina gani wanaotaga vizur na wanapatikana hapa Bongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…