Wakuu kwa mara nyingine nimefanikiwa kuagiza hawa vifaranga wa Kuroiler. Hawa ni kuku kutoka India na wanaweza fugwa free range na hawa like Dorep wanakuwa wakubwa sana. So by mwezi wa 12 nitaanza kutoa supply ya kwanza ya hawa kuku.
Mkuu inaonekana unaamini sana vitu kutoka nje,lakini kwa uzoefu wangu ni kwamba unaweza ukawa umeagiza kutoka India na bado usipate F1 ,ukaletewa F3 au ukaletewa back crossing ya parent breed kutoka F1,kwanini usiwe mbunifu ukazalisha mwenyewe F1 ya Kuroiler kwa crossing ya majogoo ya coloured broiler na mitetea ya Rhode Island Red ?au majogoo ya White leghorn ukaya - cross na mitetea ya Rhode Island Reds?
Na unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kufanya crossing ya F1 na mojawapo ya parents hapo juu ili upate sifa unazozitaka,kwa mfano kama unataka breed ambayo itakuwa ni kuroiler lakini yenye sifa nyingi za White leghorn utafanya hivi:
F1 X White leghorn = BC1white leghorn
hiyo BC1 white leghorn inamaanisha Back Crossing to parent Line of White leghorn.,kwa kutumia njia hii unaweza hata kuamua rangi ya kuroiler wako iweje.ufugaji ni ubunifu na unaweza ukatengeneza breed yako ambayo inaendana na mazingira yako na ikastawi kuliko hata hao kuroile unaowasubiria kutoka India.by the way hawa kuroiler kama jina lao linavyoonekana wametokana na BROILER kabisa sema wameongezewa tabia za Rhode island red ili waweze kutaga,wawe na tabia za kienyeji na vile vile wawe wazito.
Lastly nimeona unazungumzia pia 'F' au 'Fillial' kwenye Black Australorp maarufu kama kuku wa malawi,kwanza nikujulishe tu kuwa hawa kuku wa malawi sio chotara kama walivyo Kuroiler,Kari,kenbro,Rainbow roster,Sasso n.k, hawa ni pure breed kama walivyo White/blue/black leghorn,RIR,au Light susex.hivyo waondoe kabisa kwenye kundi la kuku chotara maana hawa ni kienyeji pure na vile vile ndio parent breed.