Kuku alitumbukia kwenye shimo la choo akakua mkubwa wamemtoa na watu wamemla

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Mtaani Kuna vituko sana sijui niseme ni uchu wa nyama ama ni sahihi.stori ipo hivi Kuna jamaa mfugaji mwenzangu yeye kuku wake alitumbukia kwenye shimo la choo Tena ni jogoo na alitumbukia akiwa mdogo basi ame survive kule ndani karibia miezi sita MPAka akaanza kuwika ndipo yule mwenye kuku akaitisha watu kwamba anayemtaka huyo kuku amchukue amtoe kweli asee walimwengu wakafanya mbinu wakatoa jogoo linene hilo watu bwana wameenda kumuosha wakampiga soap kweli akachinjwa na watu wamemtafuna walikuwa ni walevi wawili.we ungeweza kumla kuku aliyeishi katika shimo la kinyesi?
 
Hahaaa acha mkuu....njaa haina baunsa.
 
We hao kuku unaokula mitaani huko kila siku unajua walikofugiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…