Kuku wa giligiliani na chovyo ya asali

Kuku wa giligiliani na chovyo ya asali

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.


Imezoeleka kua nyama huwekewa chumvi na si sukari au asali.Hapa jikoni leo Nyama italiwa na chovyo la asali.Ni chakula ambacho kila mtu hapa jikoni anakipenda.Naamini Utakipenda pia.

Mahitaji

  • Kuku kilo 1,chemsha na chumvi na kitunguu swaumu.
Moja:kuku

  • Unga wa ngano vijiko 6 vya chakula
  • Myai matatu
  • Giligiliani Vijiko 2 vya chai.ponda view laini sana
  • Vitunguu maji vijiko 3 vya chakula,kata vipande vidogo sana
  • Pilipili manga ½ kijiko cha chai
  • Maji robo kikombe (tumia kwa awamu)
Mafuta vikombe 3 ,yakukaangia
Mbili:Chovyo

  • Asali ½ kikombe
  • Tangawizi ya unga vijiko 3 vya chai
  • Apple cidr vinegar vijiko 3 vya chakula
Njia
1. chemsha kuku aive na maji yote yakauke,acha apoe
2.katika bakuli kubwa weka mahitaji yote ya namba moja,changanya adi upate uji mzito na laini.
3.Bandika mafuta jikoni yapate moto,yasiwe yamoto sana

  • Mafuta yakiwa yamoto sana nyama itaungua kabla haijaiva
  • Mafuta yakiwa yamoto sana ukiweka kuku mafuta huruka na yanaweza kukuunguza
  • Mafuta yakiwa yamoto sana yanafanya kuku ajae hewa na kisha kupasuka na kurusha mafuta
4.chovya kila kipande cha kuku kwenye uji wa ngano kisha kaanga ,hakikisha unaivisha pande zote nakua na rangi yadhahabu.
5.Toa kwenye mafuta weka kwenye chujio la mafuta ili kudondoshe mafuta,kisha hamisha na weka kwenye sahani iliyotandikwa karatasi safi yajikoni ili kutoa mafuta yaliyobaki.Kuku tayari
Kuandaa Chovyo
1.katika bakuli,weka mahitaji yote ya namba mbili,changanya vizuri ili kupata rojo .Chovyo tayari
Weka kuku katika sahani na chovyo katika bakuli kisha tenga kwa pamoja. Chovya kipande chakuku kwenye chovyo kisha kula.Unaweza kula na chakula chochote upendacho.hapa jikoni tulikula na karoti zakuchemsha.
 
Asante kwa pishi,weekend ntajaribu hilo chovyo.
 
Hivi vyakula unatakiwa ujaribu kibachela kwanza, unaweza kuwalisha watu kituko

Asane ritz
 
Back
Top Bottom