Kuku wa kienyeji 5000 ndani ya robo acre

Joined
Aug 22, 2017
Posts
11
Reaction score
22
Watu wengi wanaamini kwamba ufugaji na haswa wa kuku unahitaji eneo kubwa sana au mabanda makubwa sana kama nyumba ili uwe na tija ,lakini ukweli ni kwamba ndani ya eneo lenye ukubwa wa robo acre unaweza kufuga kuku wengi na kujipatia kipato kikubwa kama mtu anayefuga kwenye eneo la acre tano!

Kadiri watu wanavyoongezeka, “urban farming” inaonekana kuwa ndio muelekeo mpya wa ufugaji kwa kuzingatia upungufu wa ardhi haswa kwenye maeneo ya mjini. Changamoto iliyopo miongoni mwetu ni kutazama maeneo tunayoishi kama sehemu ya fursa katika ufugaji na kufikiria ni jinsi gani unaweza kuyaongezea thamani.

Ikumbukwe kuwa soko kubwa la kuu linapatikana mjini na haswa kwenye majiji makubwa kama Dar es salaam hivyo kwa aina hii ya ufugaji ni wazi kwamba utakuwa karibu sana na soko na uangalizi wa kuku wako utakuwa ni mzuri kwa kuwa upo karibu nao muda mwingi.

JINSI YA KUFANYA
Siri kubwa katika ufugaji wa aina hii ipo kwenye utengenezwaji wa mabanda yatakayoweza kuchukua nafasi kidogo lakini kuku wengi,’Vertical farming ‘ au ufugaji wa wima ni njia inayotumika katika ufugaji wa aina hii kwa kujenga mabanda kwa kwenda juu na sio kwa mlazo,vifaa vikubwa vinavyotumika ni mbao,wire mesh,chicken wire,na bati.

Mbao hutumika kwaajili ya kuepuka gharama na kulifanya banda liwe jepesi na kuweza kuamishika pindi inapobidi.

Kwa mfano unaweza kujenga banda lenye urefu wa mita 4,upana mita 2.5 na urefu kwenda juu mita 2.5 kisha ukaligawanya sehemu tatu kwenda juu likawa na ngazi tatu,ikimaanisha kuwa katika kila ngazi utakuwa na uwezo wa kufuga kuku 100 na jumla kwa ngazi tatu ni kuku 300.

Ufugaji wa aina hii ni rahisi sana kufanya usafi na unaweza pia usifanye usafi hata kwa miezi kadhaa kwa kuwa kinyesi cha kuku kinadondoka chini ya bati. Faida nyingine ya ufugaji wa aina hii ni kupunguza upotevu wa chakula kwa kuwa chakula hakichanganyiki na uchafu mwingine wowote. Watoe kuku wako nje mchana kwaajili ya mazoezi and you are done.

Anza leo,tengeneza banda lako na weka kuku 300 mahitajio ya soko la kuku bado ni makubwa sana katika miji yetu, mfano wa banda hilii ni kama linavyoonekana kwenye picha juu unaweza kutafuta fundi akutengenezee linalofanana na hilo au kama hilo na kwa vifaa utakavyoona vinapatikana kwa urahisi unapoishi.

 
sorry je banda hili linafaa pia kwa broilers
 
Kwa Kuku Wa Kienyeji tu broilers kwa eneo hilo utapata hasara ya kufa MTU.
 
Kwa Kuku Wa Kienyeji tu broilers kwa eneo hilo utapata hasara ya kufa MTU.
mkuu broiler ndio vizuri zaidi maana haya mabanda hayana tofauti na cages zinazouzwa madukani,layers kidogo ndio inaweza ikawa shida.
 
Gharama za juu kabisa za hilo banda? Hizo bati zinawekwaje hata kinyesi kishuke na kisichanyike na chakula,atleast picha za ndani ya banda tulione. Utakuwa ni msaada mkubwa sana kwangu. Niko na mpango huo, eneo kubwa tu ndo kikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa swala la gharama za hili banda ni wewe tu utajiongeza kulingana na sehemu uliyopo na ubunifu wako, kuhusu sehemu za kulia chakula tazama kwa mbele ya banda utaziona,chakula ukikiweka katika sehemu hizo hakipotei hata kidogo.
 
Nina kuku mmoja anajisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu...ni ugonjwa gani?...unaambukiza kwa kuku wengine?...nini tiba yake?

Sent from my TV
 
Kutengeneza mibanda ya hivyo kwa kuku haijakaa poa na ni upotezaji wa nafasi kuku kwasababu ni ndege huwa inapendeza unajenga banda la pembe nne harafu ndani ya banda unapanga fito kutoka chini hadi juu wao watakuwa wanadandia tu kwa kujipanga utaona banda dogo wanaingia kuku wengi Sana.

-Ndumilakuwili-
 
Dhumuni sio kuwafurahisha kuku maana kwanza hauna uwezo wa kuwafurahisha kuku,dhumuni ni kufuga kwa tija katika eneo dogo ulilonalo,achana na mambo ya kupanga fito.
 
Mkuu, mi nadhani kuku wakiwa karibu sana kama unavyoshauri, ikitokea magonjwa ya kuambukiza, hasara itakuwa kubwa sana.

Mimi sio mtaalam ila nakuunga mkono kutumia nafasi ndogo ili upate faida zaidi.
 
Picha namna fito zilivyopangwa pls

Sent from my TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…