Kuku wa ndimu MTAMU; utamu wazidi hamu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kuku wa ndimu mtamu
Kwa huyo ninayo hamu
Sitaki kula kwa zamu
Nile niishe utamu!

Kuku wa ndimu mtamu
Simhitaji mwalimu
Nile bila kulaumu
Nimle kuku wa ndimu!

Kuku wa ndimu mtamu
Kakaangwa kitaalamu
Nikaivunja saumu
Nilipozidiwa hamu.

Kuku wa ndimu mtamu
Jirani sinidhurumu
Kwa vitunguu na ndimu
Ya kuzidisha stimu!


Kuku wa ndimu mtamu
Utamu wenye wazimu
Sijivungi nina hamu
mwenye kupika adumu!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 


Hahaaahaha, MMM leo unanifanya nilale kwa raha kabisa.

Nimependa sana beti la pili.

Duuhhh!! Kweli haihitaji Mwalimu wa kufundisha kula mchuzi wa ndimu.


Karibu sana MMU, world free of political effluence, misdemeanor and tensions
 
Tugee tusiojua tuonje nasi utamu
Sio kutuelezea na kututia hamu
Maana wenye tamaa utatutia wazimu
Na tunavyokula vitageuka chachu ka ndimu!
 
kaka naomba nikuficharing kwenye singo yangu ijayo
 
Akipakwa Ndimu
Huwezi jilaumu
Mtafune kwa hamu
pia kwa mbinu
Asitafunwe kwa zamu

Ukionja huwezi laumu
hasa maeneno muhimu
kwa mtu muhimu
Asiyejua hawezi fahamu
 

Tena awe wa singida
wamtafuna pasi shda
Ukitelemshia na soda
Hasa yule wa kienyeji
 
HERI KUNG'WAKA NPYAA......:bump:
 
Kuku unayemsema, ni kuku wa aina gani
nataka nimwambie mama, amuweke kaangoni
nile bila kulalama, utamu tele mezani
Kuku unayemsema, ni kuku aina gani

Je ni kuku wa kienyeji, au ni wale wa kizungu
Nambie mwanakijiji, ubarikiwe na Mungu
Ntamsaka mpaka jiji, nimle kwa jasho langu
Kuku unayemsema, ni kuku aina gani

Hamu imeshanizidi, siwezi kuendelea
nimeshikwa na midadi, kuku namfikiria
mimi nitajitahidi, nimpate bila hila
kuku unayemsema, ni kuku aina gani
 
bora uulize na mie namaliza post za wau... lakini sijamuelewa.... kwa ajili hapa jf wallah ukisema samaki ana maana yake,,, ukisema bata ana maana yake... sasa leo ni huyo kuku bado ninjia panda..
Jamani mwamaanisha kuku gani?
 
Mkuu MKJJ,,usije ukawa umekosea jukwaa,,huyo kuku wa hii singo ni urais au??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…