Kuku wanasinzia na kutetema kisha kufa

Kuku wanasinzia na kutetema kisha kufa

tired

Senior Member
Joined
Feb 25, 2014
Posts
107
Reaction score
23
Ni vifaranga venye umri wa wiki 5, ni vifaranga vya kienyeji pure. Nimevipa Chanjo kwa kufuata utaratibu unaotakiwa. Vilevile chakula nawapa STARTER.

Kwa Jana tu vimekufa vifaranga 4

Ushauri wataalamu
 
nenda kwenye ofisi za mkuu wa wilaya yako uliopo ulizia ofsa mifugo umueleze tatizo lako atakupa ushauri mzuri namna ya kufanya,,wapo tu wanakula mishahara ya bure kuwatumia ham watumii..
 
hao itakua wanaumwa mafua me mpk kufka juz wamekufa vfaranga wangu 10
 
Kama lishe na chanjo viko vizuri, basi angalia mambo yafuatayo :- ubaridi, usafi, mzunguko wa hewa(ventilation) nafasi au ubanano (crowding). Kwa dalili hizo mbili ni vigumu kusema tatizo ni nini haswa, Ningekuapo karibu ningefanya uchunguzi kwenye hiyo mizoga kujua chanzo cha kifo (ante mortem inspection) na kushauri utibu nini. Ila kwa sasa nina hisia tu juu ya hilo tatizo linaweza kuwa ni Gumboro (Infectious Bursal Disease). Tafuta msaada uliopo karibu nawe (afisa mifugo)
 
Magonjwa ya kuku yapo mengi jambo la msingi na la kufanya kwako , kwanza hakikisha unawatambua viranga wanaoumwa ama wenye ugonjwa kisha watenge, mfano wa magonjwa ya viranga na dalili zake....1/ KIDERI dalili zake i/ kukohoa, kupumua kwa shida, ii/ mwili kukosa nguvu, iii/ shingo kujikunja, iv/ kuharisha kijani v/ kuku hufa wengi TIBA ZAKE... Chanja katika juma lao la kwanza , na chanjo ya pili wanapofikisha umri wa miezi 4 na nusu. 2.
 
Back
Top Bottom