TUANZIE HAPA:
kwa magonjwa ya kuambukiza (infectious diseases): ili ugonjwa utokee au uendelee kuwepo kwa mnyama, ni LAZIMA mambo matatu yafuatayo yawepo kwa pamoja,
1. Vijidudu sababishi (infective causative agents) mfano bakteria, virusi au protozoa.
2. Mnyama athirika (susceptible host) hii inaeleza mnyama gani anaweza kuumwa ugonjwa gani, kwa maneno mengine ni kwamba hata iweje ng'ombe hawezi kuumwa malaria. (since it is not a susceptible host of plasmodium that causes malaria)
3. Mazingira murua ya ugonjwa kutokea au kuendelea kuwepo (favourable environment for a disease to occour or persist). Hii inajumuisha hali ya hewa, lishe, hali ya usafi, makazi, menejimenti n.k.
SASA BASI, inawezekana wewe unatibu kuku wako lakini bado hauwaondoi kwenye hayo "mazingira rafiki ya ugonjwa", (unajitibu tayphoid halafu unaenda kunywa maji machafu).
ZINGATIA: chanjo kwa wakati muafaka, tiba sahihi ya ugonjwa husika, lishe bora, banda bora, menejimenti nzuri ya kuku wako, n.k
ASANTE.